July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Machali amuumbua Mlata Bungeni

Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali

Spread the love

SIKU chache baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, (Chadema) Joseph Mbilinyi, kumshambulia Mbunge wa Viti Maalum, Martha Mlata (CCM) kwamba amevunja ndoa yake, Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali amemuumbua tena mbunge huyo wa CCM. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Machali ‘alimvua nguo’ Mlata kwa kuliambia Bunge kuwa alifumaniwa na watu aliowaita wajinga akifanya ngono.

Machali alitoa kauli hiyo  wakati akiwasilisha mapendekezo yake katika muswada wa sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi wa mwaka 2015 (The Whistleblower and Witness Protection Bill 2015).

Mbunge huyo alifikia hatua ya kutoa kauli hiyo baada ya awali kumjulisha Spika Anna Makinda kwamba baadhi ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Mlata, walikuwa wakimzomea wakati anawasilisha mapendekezo ya marekebisho ya sheria katika muswada huo.

Aliposimama mara ya pili kufafanua mapendekezo yake, Machali alianza kwa kumshambulia Mlata kwa kumtaja kwa jina kwamba hana adabu.

“Martha Mlata huna adabu, unaniita mimi kichaa, wewe uliyefumaniwa na wajinga….” Amesema Machali na kuchafua hali ya hewa Bungeni kwani baadhi  ya wabunge wakilalamikia hatua hiyo, huku wengine wakishangilia.

Kuona hali ya hewa imechafuka, Spika Makinda alisimama na kuwataka wabunge wawe na busara kwani baadhi  kauli wanazotoa Bungeni, zinawavunjia heshima.

Bara baada ya muswada huo kupitishwa, Mlata aliomba mwongozo wa Spika kutaka Machali afute kauli yake au atoe ushahidi.

“Mheshimiwa Spika, wakati Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi, Machali wakati anachangia amesema mimi nimefumaniwa na wajinga. Kwa vile kauli hiyo imerekodiwa kwenye kumbukumbu halali za Bunge, naomba afute kauli yake au athibitishe madai hayo,” amesema  Mlata.

Akitoa mwongozo wake, Spika Makinda amesema wabunge wote hao, yaani Machali na Mlata wamekosa adabu kwa kutoleana maneno yasiyo na heshima.

“Mimi nawaambia kila siku, maneno ya aina hiyo hayatawaletea heshima, mimi nilikuwa nawaangalia, wote hamkufanya kazi yenu kwa adabu,” amesema  Makinda na kufunga hoja hiyo.

Wiki iliyopita Mlata alitoa kauli Bungeni ya kumshutumu Mbilinyi, maarufu kwa jina la Sugu kwamba amempoka mchumba wake wa zamani mtoto wa miaka miwili.

Mlata amesema  jambo hilo linaonesha unyanyasaji mkubwa wa kijinsia.

Kutoka na kauli hiyo, Sugu aliomba kutoa hoja maalum Bungeni kulalamikia kauli ya Mlata na kuliambia Bunge kuwa Mahakama ndiyo iliyoamuru Sugu amchukue mwanae licha ya kuwa na miaka miwili.

Alimlaumu Mlata kwa kuingilia mambo yake binafsi wakati yeye ndoa yake imevunjika na hakuna anayemsema kwa hilo.

error: Content is protected !!