January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Machali amkana Zitto

Mbunge wa Kasulu, Moses Machali (kulia) akiwa Zitto Kabwe bungeni

Spread the love

MBUNGE wa Kasulu Mjini, Mosses Machale (NCCR-Mageuzi) amesema kuwa, hana mpango wa kuhamia katika chama kipya cha ACT-Wazalendo ambacho kiongozi mkuu wake ni Zitto Kabwe.

 Mbunge huyo amezungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum juu ya kauli ya iliyonukuliwa na vyombo vya habari kutoka kwa Zitto kwamba, Machali ni kati ya wagombea ubunge ambao watapitia tiketi ya ACT-Wazalendo. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Amesema wanasiasa ambao wapo nje ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wamekuwa wakitumia jina langu kujitafutia umaarufu kutokana na habari wanazozipata kwa wananchi jinsi ninavyokubalika kwa wapiga kura wangu.

Machali amesema, si kweli kuha ana mpango wa kuhamia chama hicho kwani anakiamini chama chake na anahamini kuwa anakubalika kwa wananchi kupitia chama hicho.

“Nashangaa kusikia maneno hayo lakini ninajua ni kwanini yamekuwa yakitangazwa hizo ni mbinu za kisiasa ambazo zinalenga kuchafuana.

“Huu ni mwaka wa uchaguzi mimi siwezi kuhama chama sioni kama kuna sababu zozote za kunifanya niame.

“Mimi nipo vizuri jimboni kwangu na mimekuwa nao kwa muda wote lakini kutokana na kuwepo kwa fitina mbalimbali za kisiasa hayo ni mambo ya kawaida hivyo nataka jamii ielewe kuwa sina mpango wa kuhama,”amesema Machali.

Mbali na hilo amesema, wapo wabunge ambao wanashindwa kukaa bungeni kwa ajili ya kujadili mabo ya msingi na badala yake wanakimbilia jimboni.

Na kuwa, jambo pekee ambalo litamfanya mbunge arudi bungeni ni matendo ambayo aliwafanyia wapiga kura wakati wa kipindi chote cha miaka mitano.

Akizungumzia kauli yake ya kutogombea nafasi ya ubunge amesema, ni kweli amekuwa na maamuzi hayo kutokana na majukumu lakini bado amnatafakari kutokana na matakwa ya wananchi ambao ni wapiga kura wake.

Pamoja na mambo mengine amesema, hata kama ataona kuna umuhimu wa kugombea hatagombea nafasi hiyo kupitia chama chochote cha siasa bali atagombea kupitia chama chake cha NCCR.Mageuzi.

 “Ili bunge limekuwa ni bunge la bajeti ndiyo maana wabunge wengi wameonekana kutokutulia bungeni, na hili unaweza kuliona wakati jambo kubwa kama hili la kujadili bajeti kuu ya serikali watu hawapo.

“Mawaziri wenyewe umeona walivyokuwa wakikimbia hawapo bungeni wengi wao ni wamejikita katika mbio za urais hivyo hakuna serikali kwa maana nyingine bajeti itapitishwa kutokana na kuwepo kwa homa za uchaguzi.

“Lakini wabunge watarudi bungeni kutokana na matendo yao kama walitumia muda wao vibaya kwa sasa hawawezi kurekebisha jambo lolote,” amesema. 

error: Content is protected !!