January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Machali ahoji nyumba za askari

Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali akizungumza bungeni

Spread the love

MOSES Machali-Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), ameibana Serikali ieleze ni lini itajenga nyumba za askari katika mji wa Kasulu.

Katika swali lake lanyongeza bungeni leo, Machali amehoji ni lini serikali itaodosha adha kubwa ambayo inawakumba askari polisi na magereza kwa kukosa nyumba imara.

Amesema “wilaya ya Kasulu Mjini ina nyumba 11 tu za askari polisi wakati jumla ya askari hao ni 200.”

Awali katika swali lake la msingi, Machali alitaka kujua ni lini serikali itatenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari katika wilaya ya Kasulu kama ilivyo kwa wilaya nyingine.

“Maisha ya askari polisi na Magereza katika suala la nyumba ni duni sana wilaya ya Kasulu. Je, lini serikali itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari hao kama ilivyo kwa wilaya nyingine,” alihoji Machali.

Akijibu swali hilo, Waziri ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereila Ame Silima, amesema kuwa kwa sasa serikali ina mpango wa kujenga nyumba za askari 4,136 nchi nzima.

Amesema kati ya nyumba hizo pia wilaya ya Kasulu itapatiwa nyumba za askari licha ya kuwa mgao haujapangwa rasmi.

Kuhusu eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam ambalo Machali alitaka kujua kama limeuzwa au litabaki mikononi kwa jeshi la polisi, Silima amesema sio kweli na kwamba halitauzwa kwa mtu yoyote wala kwa mwekezaji.

Amesema mahitaji ya ujenzi wa nyumba za polisi na magereza katika nchi nzima ni kubwa na serikali haiwezi kujenga nyumba hizo kwa wakati mmoja kutokana na uhaba wa fedha.

“Kwa upande wa jeshi la polisi, serikali inatarajia kupata mkopo nafuu toka serikali ya China utakaofanikisha ujenzi wa nyumba 4,136 nchi nzima.

“Aidha, kupitia dhana ya mashirikiano ya sekta ya Umma na binafsi (PPP), jeshi la polisi chini ya shirika lake la uchumi, litajenga nyumba 350 eneo la Oysterbay,”alisema Silima.

error: Content is protected !!