Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Maboresho Bandari Tanga kufanya mapinduzi ya kiuchumi, kijamii
Habari Mchanganyiko

Maboresho Bandari Tanga kufanya mapinduzi ya kiuchumi, kijamii

Spread the love

MAMLAKA ya Bandari ya Tanga imesema maboresho ya bandari hiyo yatawezesha kupokea zaidi ya tani milioni 3 za shehena za mizigo kwa mwaka, kutoka tani 750,000, hali ambayo itachochea ukuaji wa uchumi wa nchi na wananchi. Anaripoti Selemani Msuya, Tanga … (endelea).

Hayo yamesemwa na Meneja wa Bandari hiyo, Masoud Mrisha wakati akizungumza na waandishi wa habari za uchumi, biashara na uwekezaji waliotembelea bandari hiyo jana.

Mrisha amesema Agosti 2019 Serikali iliagiza kufanyika kwa maboresho ya bandari hiyo ambapo hadi yatakapokamilika Aprili 2023 jumla ya Sh.bilioni 429.1 zitatumika.

Amesema maboresho ya bandari hiyo yatawezesha utoaji huduma kwa meli kubwa ambazo awali zilikuwa hazifiki hapo, hivyo kusababisha gharama kubwa

“Zaidi Sh.bilioni 429 zimetumika kufanya maboresho Bandari ya Tanga, matarajio yetu ni baada ya kukamilika tutaweza kupokea mzigo mwingi hadi kufikia tani milioni 3 kutoka tani laki 750,000,” amesema.

Amesema pamoja na kuongeza uwezo wa kupokea mzigo, pia mapato yataongezeka na uchumi wa Tanga, mikoa ya Kaskazini na nchi kwa ujumla utakuwa.

Mrisha amesema pia maboresho hayo yatawezesha ajira kuongezeka.

“Gharama za Mradi huu kwa awamu ya kwanza ulikuwa Sh.bilioni 172.4,″ amesema Mrisha.

Mrisha amesema maboresho hayo yamehusiha uongezaji wa kina cha maji kutoka mita tatu hadi mita 13 na upana wa mita 73 kwenye njia ya kuingiza na kutokea meli, ambapo awali mzigo ulikuwa unafutwa umbali wa kilomita 1.7 kutoka kwenye gati.

Meneja huyo amesema kwa sasa wapo katika awamu ya pili ya maboresho ya bandari ya Tanga yaliyoanza Septemba 2020 na hadi sasa yamefikia asilimia 83, yanatarajiwa kukamilika Aprili 2023 ambapo takribani bilioni 256.8 zitatumika.

Amesema awamu hiyo ya pili ya mradi imehusisha maboresho ya magati mawili yenye urefu wa mita 450.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari Mchanganyiko

GGML yasisitiza kuendelea kuimarisha afya za wafanyakazi

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na kampuni...

error: Content is protected !!