August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mabomu yarindima Mwanza

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Mwanza limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya madereva wa daladala walioanza mgomo baridi katika stendi ya mabasi yaendayo mikoani-Nyegezi, anaandika Moses Mseti.

Mgomo huo wa madereva wa daladaa zinazofanya safari zake kati ya Buhongwa na Uwanja wa Ndege, umeanza leo saa 1: 00 asubuhi hadi saa 5 asubuhi, sababu za mgomo huo ni baadhi ya madereva wa daladala kukamatwa na polisi.

Sababu ya madereva hao kukamatwa ni kudaiwa kukiuka utaratibu, kanuni na sheria za usalama barabarani ikiwemo kuegesha daladala nje ya vituo.

Petro Dede, Mwenyekiti wa Madereva wa Daladala, Kanda ya Ziwa amesema, sababu za madereva wengi kushindwa kufuata utaratibu wa kwa mujibu wa sheria ni kunatokana na kutokuwepo kwa vituo maalum vya kushusha abiria.

Amesema kuwa, tatizo la kutokuwepo vituo maalum jijini humo linasabishwa na serikali yenyewe kushindwa kuainisha vituo hivyo jambo linalozua migogoro kila kukicha.

“Kila siku ushuru unalipwa lakini barabara zote hazina alama za vituo na tukianza kulalamika, tunaonekana sisi ndio wenye makosa wakati makosa ni yao.

“Kama hawata badilisha na kuweka alama na kuainisha vituo vya kushuisha na kupakia abiri hatutanyamaza, haiwezekani makosa ni yao lakini sisi ndio tutozwe faini,” amesema Dede.

Daniel Chilongani, Ofisa wa Mamlaka ya Usafirishaji Nchi Kavu na Majini (Sumatra) mkoani humo amesema kuwa, chanzo cha mgomo huo baridi ni kutokana na ukosefu wa vituo vya kupakia abiria.

Hata hivyo, Chilongani amesema kutokana na tatizo hilo, atakwenda kuueleza uongozi wa Sumatra ili kuangalia ni namna gani wanaweza kulipatia ufumbuzi suala hilo.

Mmoja wa madereva hao, Shaban Ntolo amesema kuwa, wamechoka na unyanyasi unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoani humo.

“Leo ngoja turudishe gari barabarani ili kuwasaidia Wananchi ambao ndio wanaopata usumbufu na muda huu tukiwa tunasubiri majibu kutoka kwa viongozi wetu,” amesema Ntolo.

error: Content is protected !!