Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Habari Siasa Mabilioni yaibwa kwa Jaji Mutungi
SiasaTangulizi

Mabilioni yaibwa kwa Jaji Mutungi

Spread the love

MAMILIONI ya shilingi ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa yaliyotengwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake ndani ya vyama vya siasa nchini, hayajulikani yalipo, anaandika Shabani Matutu.

“Ama mamilioni hayo yamekwapuliwa au yametumika isivyopasa,” MwanaHALISI limeelezwa.

Taarifa kutoka ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa zinasema, mamilioni hayo ya shilingi yaliingizwa katika akaunti ya Msajili katika benki lakini sasa hayajulikani yalipo au yalivyotumika.

Mmoja wa maofisa waandamizi ndani ya ofisi ya waziri mkuu ameliambia gazeti hili kuwa tayari uchunguzi umeanza ili kufahamu jinsi  fedha hizo zilivyotumika.

Mtoa taarifa huyo anasema, “kuyeyuka” kwa fedha hizo kuligunduliwa na mkaguzi wa ndani wa ofisi hiyo.

Amesema, “ofisi ya msajili ilipokea Sh. 600 milioni ili zitumike kujengea uwezo wanawake ndani ya vyama vya siasa; lakini kazi hiyo haijafanyika.”

Amesema, “…baada ya kubaini kutokuwepo fedha hizo au ushahidi wa matumizi yake, ndipo ikaagizwa ufanyike ukaguzi maalum ili kupata uhakika wa kile kilichoonwa na mkaguzi wa ndani.”

MwanaHALISI lilipomuuliza Jaji Francis Mutungi juu ya madai ya kupotea kwa mamilioni hayo ya shilingi, alikiri kuwapo ukaguzi katika ofisi yake kuhusiana na upotevu wa fedha hizo.

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari za SiasaTangulizi

Wabunge wacharuka kukatika kwa umeme

Spread the loveTATIZO la kukatika kwa umeme kila mara katika maeneo mbalimbali...

Habari za SiasaTangulizi

Watu 1,673 wamchangia Lissu Sh. 20 milioni kununua gari

Spread the loveWATU 1,673 wamechanga fedha zaidi ya Sh. 20 milioni kwa...

Habari MchanganyikoTangulizi

11 wafariki dunia baada ya mtambo wa Kiwanda cha Mtibwa Sugar kupasuka

Spread the loveWATU 11 wamefariki dunia huku watatu wakijeruhiwa katika ajali ya...

error: Content is protected !!