August 12, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mabasi ya kampuni moja yaua 27

Spread the love

WATU 27 wamefariki dunia kutokana na ajali mbaya ya mabasi mawili ya kampuni moja kugongana uso kwa uso katika eneo la Maweni wilayani Manyoni Mkoani Singida, anaandika Dany Tibason.

Kwa mujibu wa maelezo ya Thobias Sendoyeka, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singiga, amesema waliokufa ni 27 kati yao wanaume 19 na wanawake ni 8.

Kamanda Sendokaya amesema mabasi yaliyogongani ni ya kampuni ya City Boys lenye namba za usajili T541 BCE lililokuwa likitokea Dar es Saalam kuelekea Kahama.

Amelitaja basi lingine la kampuni hiyo ni City Boys lenye namba za usajili T247 ABD lililokuwa likitokea Kahama kuelekea Jijini Dar es Salaam.

Kamanda Sondeyeka amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana kutokana na kuwepo kwa mwendo kasi.

Amesema mpaka sasa majeruhi hawajajulikana kutokana na ukubwa wa ajali na kuongeza kuwa baadhi ya majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya wilaya Manyoni huku wengine wakikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Amesema kwa mujibu wa mashuhuda wamesema kuwa madereva hao walionekana kuyumba barabarani kama ishara ya kusalimiana jambo ambalo lilisababisha kutokea kwa ajali hiyo mbaya.

Hata hivyo amesema baada ya kumaliza huduma zote kwa waliopata ajali atatoa taarifa zaidi katika vyombo vya habari.

error: Content is protected !!