August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Mabaraza ya Ardhi yaimarishwe’

Spread the love

SERIKALI imetakiwa kuhakikisha Mabaraza ya Ardhi yanaimarishwa kwa kuongeza kasi ya uundaji wa mabaraza mapya na kuyawezesha ili yafanye kazi kwa ufasaha, anaandika Pendo Omary.

Hatua ya serikali kuimarisha mabaraza hayo itasaidia kukabikiana na changamoto za mazingira yasiyoridhisha ikiwemo ukosefu wa ofisi, maktaba na vitendea kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Amina Rashid, Kaimu Msajili Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya amesema mabaraza hayo yanakabikiwa na upungufu wa watumishi.

Watumishi hao ni wenyeviti, makarani na wapiga chapa hali inayochelewesha kusikilizwa kwa mashauri yaliyofunguliwa na wananchi kutopata nakala za hukumu na mienendo ya mashauri kwa wakati.

“Kasi ndogo ya uundaji wa mabaraza ya ardhi, kuchelewa kufanyika kwa ukaguzi wa maeneo ya migogoro kutokana na ukosefu wa usafiri na uelewa mdogo wa wananchi juu ya Sheria ya Kanuni za uendeshaji wa migogoro zimekuwa ni changamoto kuu katika mabaraza haya,” amesema Amina.

Amina amesema ili kukabikiana na changamoto hizo, serikali inapaswa mabaraza yanakuwa na ofisi zinazostahili na za kutosha, wenyeviti wawili au watatu kwa mabaraza yenye mashauri mengi.

Pia kuyapa fedha za kutosha za uendeshaji na kuweka mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya kutunza kumbukumbu na kielimisha wananchi kuhusu Sheria ya mahakama za ardhi ya mwaka 2002 na kanuni za mabaraza za mwaka 2003.

error: Content is protected !!