
Spread the love
RAIS John Magufuli amewataka mabalozi wa Tanzania katika nchi za nje ambao hawajatumia vyema madaraka yao katika kuiletea nchi maendeleo, kujiandaa kurudi nyumbani. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).
Rais Magufuli ameyasema hayo katika hafla ya uapisho wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro iliyofanyika leo tarehe 29 Septemba 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Maguguli amewataka mabalozi hao kuwa na desturi ya kuwasilisha ripoti kuhusu kazi walizofanya kwenye vituo vyao vya kazi.
“Mabalozi wa Tanzania walioko nje wawe wanaeleza wamefanya nini na kama hawajafanya kitu wajiandae kurudi,” amesema Rais Magufuli.
More Stories
Mrithi wa Maalim Seif, siri nzito
Rais Magufuli amuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya
Dk. Bashiru: Nilipata taarifa za uteuzi mitandaoni