Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mabalozi wamchambua Rais Samia
Habari Mchanganyiko

Mabalozi wamchambua Rais Samia

Spread the love

 

MABALOZI wa nchi mbalimbali nchini Tanzania, wametumia sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kuuelezea uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Ijumaa, tarehe 13 Aprili 2022, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali ikiwemo viongozi wa kiserikali, asasi za kiraia, mabalozi na watetezi wa haki za binadamu ambapo Rais Samia, alikuwa mgeni rasmi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Peter Van Acker, amesema uongozi wa Rais Samia umeleta mabadiliko makubwa ndani ya muda mfupo katika uimarishwaji wa haki za binadamu ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza.

“Rais wa Tanzania alikuwa Arusha katika maadhimisho ya siku ya habari duniani na nafikiri alizungumza kitu kuhusu kukaribisha majadiliano na kuhakikisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na Serikali, nafikiri hili ni jambo chanya,” amesema Balozi Van Acker.

“Sasa tunaamini sheria mbalimbali za habari zitarekebishwa kwa sababu baadhi yake nafikiri zilikuwa mbaya na zinakwenda kinyume na Ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania. Itakuwa pia ni muhimu sheria zinazosimamia siasa za nchi na asasi za kiraia na taasisi za haki za binadamu zikabadilishwa ili ziwe nzuri,” amesema Van Acker.

Akizungumzia miaka 10 ya THTRDC, Van Acker amesema “nimekuja hapa kumalizia kipindi changu cha mwisho Tanzania sababu ni miaka minne tayari na nitaondoka hivi karibuni. Lakini kuishi kwangu Tanzania nimeona dalili nyingi chanya na maendeleo chanya. Na nimekuwa shuhuda wa safari ya miaka 10 ya THRDC.”

Balozi Van Acker amesema THRDC licha ya kufungiwa akaunti zake za benki na uongozi wa Awamu ya Tano, uliendelea kutekeleza majukumu yake kwa msaada wa Rais Samia.

“Safari ya THRDC naiona ni nzuri sababu licha ya kufungiwa akaunti zake za benki lakini iliendelea kufanya kazi na sasa tuko hapa kwa support ya Rais Samia aliyewakilishwa hapa na Waziri. Nafikiri muda umebadilika kweli ndani ya muda mfupi,” amesema Balozi Van Acker.

Kwa upande wake Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Emilio, amefurahishwa na kitendo cha Serikali ya Rais Samia kufungua milango ya majadiliano hususan ya kisiasa, ambayo yameleta mabadiliko katika masuala ya haki za msingi za binadamu.

“EU ni mshirika katika kuunga mkono haki za binadamu Tanzania kwenye ngazi zote, kwanza tumeanza na majadiliano ya siasa na Serikali ambayo tuna furaha tumeweza kurejesha mabadiliko 2021 ambayo yanajumuisha haki za msingi za binadamu na tunaendelea na makubaliano ya kushirikiana na taasisi za Serikali na asasi za kiraia,” amesema Balozi Emilio.

Naye Balozi wa Norwey nchini Tanzania, Elisabeth Jacobesen, ametoa ushauri kwa asasi za kiraia akizitaka ziendelee kuimarisha hali ya haki za binadamu nchini, hususan haki za kidemokrasia na uhuru wa kujieleza.

“Nina jumbe tatu kwenu kwa siku ya leo, wa kwanza tunawatia moyo muendelee na jitihada za kuchochea na kuimarisha haki za binadamu. Tunahitaji muendelee na kazi hiyo na natumia nafasi hii kuwatia moyo muendelee na kazi hiyo katika kutetea haki za demokrasia, uhuru wa kujieleza na kiraia na utawala bora wa sheria-Balozi Jacobesen.

1 Comment

  • o mabalozi watakuwa wamefurahi kwa sababu yumkini ndio waliogharamia mkutano huo mzima pamoja na posho na mshiko kwa washirika. Tegemezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

Habari Mchanganyiko

Bodi ya Maji Wami Ruvu kuchimba visima 10 kupunguza uhaba maji mikoa mitatu

Spread the love  BODI ya Maji ya Bonde la Wami Ruvu imesema...

Habari Mchanganyiko

NBC Dodoma International Marathon kutimua vumbi Julai 23

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetanganza msimu wa nne...

error: Content is protected !!