UONGOZI wa klabu ya Yanga upo mbioni kuitisha mkutano mkuu wa wanachama hivi karibuni huku moja ya ajenda ikiwa ni mabadiliko ya katiba kuelekea mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endela).
Rasimu hiyo ya mabadiliko ilikabidhiwa Desemba 2020, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Mabadiliko ya Uendeshaji wa Klabu ya Yanga, Wakili Alex Mgongolwa na kukabidhiwa Dk. Mshindo Msolwa ambaye ni Mwenyekiti wa Yanga.
Mara baada ya kukabidhiwa Rasimu hiyo, Msolla alisema kinachofuata kwa sasa ni kukutana na viongozi wa matawi na kuwapa elimu juu ya mfumo huo wa mabadiliko na baadaye kuitisha mkutano wa wanachama kwa ajili ya mabadiliko ya katiba.
Taarifa iliyotolea leo na klabu ya Yanga, imeeleza kuwa uongozi huo unajipanga kuitisha mkutano wa wanachama hivi karibuni na kuwataka wanachama kulipia kadi zao kwa njia mbalimbali ili waweze kupata uhalali wa kuingia kwenye mkutano.
Yanga itakuwa klabu ya pili kuingia kwenye mfumo huo wa kisasa wa uendeshaji wa klabu kwa kukaribisha uwekezaji kupitia manunuzi ya hisa kama ilivyokuwa kwa wenzao Simba.
Leave a comment