January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mabadiliko yaja baraza la mawaziri Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anaweza muda wowote kuanzia sasa, akafanyika mabadiliko makubwa ndani ya Baraza lake la Mawaziri. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka serikalini na ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zinaeleza kuwa Rais anaweza kufanya hivyo, ili kukidhi mahitaji ya utendaji kazi wa Serikali yake.

Aidha, mabadiliko hayo, yanatokana na hatua ya Rais Samia, kutangaza kuigawa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kuunda wizara mbili – Wizara ya Afya na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Vilevile, mabadiliko hayo, yanatokana na kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), William ole Nasha, ambaye alikuwa mbunge wa Ngorongoro, Arusha.

Nasha alifariki dunia Jumatatu, 27 Septemba 2021 akiwa Dodoma.

Undani wa habari hii, soma gazeti la Raia Mwema la leo Jumatatu, 3 Januari 2022

error: Content is protected !!