August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mabadiliko katika sekta ya madini

James mdoe, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini

Spread the love

Wizara ya Nishati na Madini imefanya mabadiliko kufuatia kupitishwa kwa sheria mpya ‘the written laws (miscellaneous amendmend ) Act 2017  iliyofanyiwa marekebisho kadhaa katika sheria ya mwaka 2010, anaandika Victoria Chance.

Marekebisho hayo ni kuanzishwa kwa tume ya madini, kufutwa kwa wakala wa ukaguzi wa madini, kuongezeka kwa malipo ya mrabaha asilimia nne(4%) hadi asiliia sita(6%), kwa madini ya metali na kuongeza kwa  kwa malipo ya mrabaha kutoka asilimia tano(5%) hadi sita(6%) kwa almasi na vito.

Pia kupitia marekebisho ya sheria ya fedha  na kodi, kila kampuni au mtu atakayesafirisha madini nje atalipia  ada ya ukaguzi ambayo ni asilimia moja ya thamani ya madini yake na hata wachimbaji wadogo  watalipia asilimia tano (5%) ya thamani ya madini yake ikiwa kama  kodi ya zuio.

Aidha, katika suala la kufutwa kwa  TMAA na ofisi za madini za kanda  wizara imesema watumishi wataendele  kufanya kazi kwani hawana tuhuma zozote na katika kipindi ambapo tume ya madini haijaundwa  shughuli za tume  zitafanywa chini ya kamishna wa madini .

Hata hivyo, wizara imewasisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano hasa katika  kipindi hiki cha mpito wakati serikali imesimamisha utoaji wa leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini hadi hapo tume ya madini itakapoundwa.

error: Content is protected !!