Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Maaskofu wambebesha mizigo Rais Samia
Habari MchanganyikoTangulizi

Maaskofu wambebesha mizigo Rais Samia

Rais wa TEC, Askofu Mkuu, Gervas Nyaisonga
Spread the love

 

BARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limemuomba Rais wa Awamu ya Sita, Samia Suluhu Hassan, apitie upya sera ya ushirikiano baina ya Taasisi za Dini na Serikali, ili kuondoa vikwazo vinavyokwamisha taasisi hizo kutoa huduma za kijamii. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ombi hilo limetolewa leo Ijumaa, tarehe 25 Juni 2021 na Rais wa TEC, Askofu Mkuu, Gervas Nyaisonga, katika mkutano wa Rais Samia na Maaskofu Katoliki, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

“Tunakuomba Serikali yako ifanye upya mapitio ya sera ya ushirikiano, baina ya mashirika ya dini na Serikali ili kwa pamoja tulenge kutatua matatizo ya wananchi, hasa katika maeneo yenye uhitaji mkubwa na si kuendeleza maeneo ambayo tayari yana uwekezaji wa mashirika ya dini,” amesema Askofu Nyaisonga.

Askofu Nyaisonga ametoa ombi hilo akisema, tangu 2016 sera za ushirkiano baina ya Serikali na taasisi hizo, zilibadilika hali iliyokwamisha taasisi hizo kufanya majukumu yao ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

“Rais mnamo 2016, sera mbalimbali zilibadilika na kutukwamisha kuendelea kutoa baadhi ya huduma kwa ufanisi, hasa kwenye sekta ya elimu ya juu, bila kujali uwekezaji mkubwa uliofanywa na kanisa kabla ya hapo,” amesema Askofu Nyaisonga.

Askofu Nyaisonga amesema “ hii ilisababisha hasara kubwa ya kifedha na hata rasilimali nyingine zilizokuwa zimewekezwa ikiwa pamoja rasilimali watu, madhara yake yamekuwa makubwa kitaasisi yamedhoofisha huduma hizo ikiwa pamoja maslahi ya watumishi na tozo husika za Serikali kutolipwa kwa wakati.”

Rais huyo wa TEC amesema, mabadiliko ya sera hizo yameathiri kwa kiasi kikubwa uwekezaji wa taasisi za dini katika elimu ya juu na sekta ya afya.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

“Mabadiliko haya yamesababisha kupungua wanafunzi katika taasisi za elimu ya juu kutokana na madhara ya sera hizo kwenye udahili wa wanafunzi. Wataalamu wetu walipungukiwa moyo wa kujitoa katika kuhudumia Watanzania, wengine kuondoka kwenda katika maslahi zaidi na kudhoofisha huduma zote,” amesema Askofu Nyaisonga.

Pia, Askofu Nyaisonga ameiomba Serikali ya Rais Samia, kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), isamehe madeni ya kodi ambazo taasisi hizo zinadaiwa, ili zieweze kukabiliana na changamoto za kifedha hususani katika kipindi cha mlipuko wa Virusi vya Corona (Covid-19).

“Tunaomba Serikali kupitia TRA itoe msamaha wa kodi na riba yake, kwa taasisi ya afya na elimu za mashirika ya dini kwa miaka ya nyuma, kabla ya kutekelezwa sheria mpya ya fedha ya 2021/22, hii itawezesha uongozi na taasisi hizi kujikita kuboresha huduma hasa katika kipindi kigumu cha Covid-19,” amesema Askofu Nyaisonga.

1 Comment

  • Asasi za kidini nyingi zimekuwa zikidanganya na kupata msamaha wa kodi Hii haikubaliki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

error: Content is protected !!