Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Maaskofu Katoliki watahadharisha maambukizi ya corona
AfyaHabari MchanganyikoTangulizi

Maaskofu Katoliki watahadharisha maambukizi ya corona

Spread the love

 

BARAZA la Maaskofu la Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), limetoa tahadhari kwa wananchi kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona na ugonjwa wa uviko (COVID-19). Anaripoti Saed Kubenea, Dar es Salaam … (endelea).

Waraka wa kanisa hilo, uliotumwa kwa Mwadhama, Mpelekwa wa Baba Mtakatifu, Maaskofu Wakuu, Maaskofu na Maaskofu Wastaafu, umeeleza kuwapo wimbi jipya la maambukizi ya Korona ulimwenguni na hivyo, ni muhimu kujikinga na ugonjwa huo.

Waraka wa TEC, umesainiwa na rais wake, Gervas Nyaisonga, ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Mbeya. Umepewa kichwa cha maneno kisemacho: “Tahadhari juu ya maambukizi mapya ya virusi vya Korona na ugonjwa wa Uviko 19 (COVID 19.”

Askofu Nyaisonga anasema, kuna wimbi jipya la maambukizo ya Korona kufuatia nchi kadhaa kuthibitisha kupita kwenye kipindi kigumu cha kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo.

Waraka wa TEC kwenda kwa maakofu umerekodiwa kwa kupewa kumbu Na. TEC/PR/2021/02 la tarehe 26 Januari mwaka huu.

Amesema, “nchi yetu siyo kisiwa. Hatuna budi kuzingatia hekima ya wahenga wanasema, mwenzio akinyolewa wewe wewe tia maji. Ni muhimu tukaendelea kuzingatia kanuni za afya katika kukohoa au kupiga chafya na kuepuka kusogeleana, kugusana na kusongamana.”

Anasema, “hatuna budi kujihami, kuchukua tahadhari na kumlilia Mungu kwa nguvu zaidi, ili janga hili lisitukumbe.”

Rais wa TEC, anazidi kueleza maaskofu wenzake, kwamba “kwa uhalisia huo, tusiache kuwashauri, kuwahimiza na kuwaongoza taifa la Mungu katika mapambano haya dhidi ya virusi vya Korona.”

Anasema, “tusichoke kuhimiza sala, kuepuka kugusana, kunawa na kujitakasa kila wakati, kuchukua hatua tuonapo dalili za ugonjwa na kuepuka msongamano hatarishi.” 

Katibu wa TEC, Padre Charles Kitima, akizungumza na MwanaHALISI Online, kuhusu tahadhari hiyo amesema, “hiyo ni barua ya kiongozi wa Kanisa, anawaandikia maskofu wenzake, akiwashauri kuchukua tahadhari ya ugonjwa huu.”

Waraka wa TEC kwa maaskofu, umekuja takribani wiki moja tokea Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Isaac Aman, kutoa andishi la kura mbili akitaka wananchi kutomjaribu Mungu katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona. 

Katika andishi hilo alilolituma na kulisoma kwa kwa waumini wake, Askofu Amani anasema, “…tusimjaribu Mungu kwa kufanya uzembe na maisha yetu. Turejee tahadhari za kuzuia maambukizi bila ya kuwa na hofu.”

Askofu Isaac Aman, wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha

Waraka wa Askofu Amani ameupa kichwa cha maneno kisemacho, “Kutembea Pekupeku Juu ya Mbigili.”

Anasema, watu wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuwa ugonjwa huo upo na unatesa mataifa mengi duniani.

“Maji ya kunawa kanisani yameondolewa, na pengine yapo lakini watu hawanawi tena kwa imani kwamba hakuna Korona. Hata ile tahadhari ya kutoshikana mikono watu wamejiondolea wenyewe kwa imani kwamba, hakuna Korona,” ameeleza.

Amesema, taifa linalazimika kutengeneza utamaduni mpya, huku akitahadharisha kuwa jamii inapaswa kutafakari upya kwa kuwa “mwenendo wake wa sasa, unatia mashaka.”

Askofu huyo mashuhuri nchini amewataka mapadri na watawa kuchukua tahadhari, huku akisisitiza umuhimu wa kila mmoja kuchukua tahadhari kwa manufaa yake na wengine.

Aidha, hatua ya TEC kutoa tahadhari  kujikinga na Korona inakuja wakati takwimu zilizotolewa na taasisi ya World Meter, zinaeleza kuwa maambukzi ya virusi vya corona (COVID-19) duniani, yamefikia watu 100.4 milioni.

Shirika hilo linataja waliofariki kwa ugonjwa huo ulimwenguni, wamefikia watu 2.15 milioni, huku waliopona wakikadiriwa kuwa watu 72.39 milioni.

Hadi leo mchana Jumanne tarehe 26 Januari 2021, mtandao wa World Meter unaonyesha Marekani inaongoza kwa maambukizo kwa kufikia watu 25.86 milioni. Waliofariki kwa ugonjwa huo, wanatajwa kuwa ni watu 431,392 na waliopona 15.61 milioni.

Taifa la India linashika nafasi ya pili duniani ikiwa na maambukizo 10.6 milioni. Waliokufa wanakadiriwa kuwa watu 153,624 na waliopona 10.34 milioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!