Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Maaskofu: Anayekwepa kuhesabiwa ni mtenda dhambi
Habari Mchanganyiko

Maaskofu: Anayekwepa kuhesabiwa ni mtenda dhambi

Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu wa makanisa ya Kipentekosti Tanzania, Askofu Peter Konki
Spread the love

 

BARAZA la Maaskofu wa Kanisa la Kipentecost Tanzania (CPCT) limesema litawahamasisha waumini wake na kuwapatia elimu juu ya umuhimu wa kujitokeza wakati wa sensa ya watu na makazi itakayofanyika mawaka huu Agosti 23 mwaka huu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma …  (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 11 June, 2022 na Mwenyekiti wa Baraza la maaskofu wa makanisa ya Kipentekosti Tanzania, Askofu Peter Konki alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu ulioambatana na uchaguzi mkuu wa kikatiba uliofanyika Dodoma.

Amesema waumini wa kanisa hilo wanatakiwa kutambua umuhimu wa sensa ya watu na makazi kwani ni haki ya serikali kutambua watu ambao wapo nchini.

Kutokana na hali hiyo basi ni wajibu wa kila kiongozi wa kanisa letu kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuhesabiwa na pasiwepo na kikwazo chochote wakati ukifika.

“Suala la kuhesabiwa ni muhimu sana kwa taifa kwa maana ni lazima serikali itambue na kujua idadi yao ili kuweza kujua ni namna gani ya kuweza kuwahudumia.

” Suala la sensa halikuanza leo hata wakati wa ufalme kabla ya Yesu kuzaliwa suala la kuhesabiwa lilikuwepo kwa hiyo mtu ambaye anakwepa kuhesabiwa ni mtenda dhambi kwani anakwamisha juhudi za kuhesabiwa yeye” amesema Askofu Konki.

Amesema kuwa watanzania wanatakiwa kutambua umujimu wa sensa kwani sensa ni dira pekee ya kuifanya serikali kutambua ina watu wangapi kwa makundi hani na wenye uhitaji gani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

Habari Mchanganyiko

NMB yafuturisha Dar, Majaliwa azitaka Serikali za Mitaa, Taasisi zijifunze kwao

Spread the loveBENKI ya NMB imewafuturisha wateja wake walio kwenye Mfungo wa...

error: Content is protected !!