May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maangamizi Myanmar, waliouawa wafika 126

Spread the love

 

IDADI ya wananchi waliouawa nchini Myanmar tangu jeshi la nchi hiyo kupora madaraka na kuanza kwa mandamano tarehe 1 Februari 2021, wamefika 126. Inaripoti Aljazeera…(endelea).

Jeshi la nchi hiyo, linaendeleza mauaji kwa raia wa nchi hiyo wanaopinga utawala wa kijeshi, baada ya viongozi wa juu wa taifa hilo kuwekwa kizuizini.

Miongoni mwa viongozi wanaoshinikizwa kuachiwa huru ni pamoja na kiongozi wa upinzania Aung San Suu Kyi, ambaye aliingia madarakani kwa kuchaguliwa.

Christine Schraner Burgener, Mjumbe wa Umoja wa Mataifa (UN), nchini Myanmar amesema, kanda za video za mauaji zinatisha, na kwamba polisi wamekuwa wakituma risasi za moto.

Tayari Marekani na Uingereza zimelaani nguvu kubwa inayotumiwa na jeshi hilo kuyakabili maandamano hayo. Hata hivyo, Serikali ya Kijeshi Myanmar imekuwa ikipuuzia wito wa kusitisha mauaji.

Jumatano wiki iliyopita, inaelezwa na mjumbe huyo wa UN, kwamba ilikuwa ya maangamizi makubwa. Ni baada ya watu 38 kuuawa ndani ya saa 24.

Taarifa zinaeleza, mashambulizi ya jeshi hilo yamekuwa yakiwaathiri madaktari na wasaidizi kutoka kitengo cha afya huduma kwa watu waliojeruhiwa.
Pia, mashambulizi hayo yamekuwa yakiwaacha na majeraha wajenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajenzi wa barabara.

“Ukatili unaoendelea, umekuwa ukiwaumiza matabibu na wale wanaofanya shughuli za ujenzi wa miundombini. Lakini watu wanaandamana kwa amani tu,” amesema Burgener wa UN.

Mwanafunzi mmoja katika Mji wa Mandalay, ameripoti kwamba jeshi hilo limekuwa likifyatua risasi za mpira na za moto kwa pamoja pale wanapoona kundi la watu wanaojikusanya karibu na nyumba zao.

YANGON, MYANMAR – MARCH 01: Anti-coup protesters shout slogans on March 01, 2021 in Yangon, Myanmar. Myanmar’s military government has intensified a crackdown on protesters in recent days, using tear gas and live ammunition, charging at and arresting protesters and journalists. At least 18 people have been killed so far, according to monitoring organizations. (Photo by Hkun Lat/Getty Images)

“Nadhani kama mwendo wa saa nne au nne na nusu asubuhi, polisi na walifika katika eneo hilo na kisha wakaanza kuwapiga risasi raia. Hawakutoa onyo lolote kwa raia.

“Walitokea tu na kuanza kupiga risasi. Walitumia risasi za mpira na pia risasi halisi kuua raia kwa njia ya kikatili,” ameeeleza.

Jeshi la Myanmar lilieleza sababu za kufanya mapinduzi baada ya uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia kufanyika ambapo Suu Kyi wa chama cha upinzani – NLD kushinda.

Jeshi hilo lilieleza, uchaguzi huo uliofanyika Novemba 2020, uligubikwa na ulaghai. Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo ilipinga madai hayo, sasa imetangaza kufanyika kwa uchaguzi upya lakini haijapanga tarehe rasmi.

error: Content is protected !!