May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maambukizi mapya ya Ukimwi yatafuna vijana

Spread the love

 

TAFITI zilizofanywa na Tume ya Kudhibiti Ugonjwa wa Upungufu wa Kinga Mwilini (Ukimwi) nchini Tanzania (TACAIDS), zinaonesha takribani watu 7,7000 wanapata maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa mwaka, huku kundi la vijana likiongozwa kuathirika na janga hilo.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumamosi, tarehe 14 Agosti 2021 na Mkurugenzi wa Habari TACAIDS, Jumanne Isango, akizungumza na wanahabari kuhusu wiki ya vijana , jijini Dar es Salaam.

Isango amesema, kati ya idadi hiyo ya maambukizi mapya, asilimia 40 ni vijana. Kati ya vijana hao, asilimia 80 ni wa kike.

“Takwimu ambazo tumekuwa tukizfanya mara kwa mara zinaonesha kuna watu 77,000 wanapata Ukimwi kwa mwaka. Kati yao asilimia 40 ni vijana ambao wanapata maambukizi mapya, kati ya aisilimia hizo 40, asilimia 80 ni wanawake, kati ya umri wa miaka 15 mpaka 24,” amesema Isango.

Kufuatia changamoto hiyo, Isango amesema TACAIDS imeandaa kampeni maalumu ya kutoa elimu kwa umma hasa vijana, juu ya kujikinga na Ukimwi.

“Tuna kampeni mbalimbali ambazo zimeshafanyika na zinaendelea. Hivi karibuni tuna kampeni ambayo itaanza rasmi mwezi huu, siku chache zijazo itaanza. Inatwa ‘Ongea’ itakayohusisha redio kubwa,” amesema Isango na kuongeza:

“Kampeni hii ya vijana itaelezea kinga dhidi ya Ukimwi, mimba zisizotarajiwa, ukatili wa kijinsia na maeneo kama hayo.”

error: Content is protected !!