Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Maambukizi malaria yapungua
Afya

Maambukizi malaria yapungua

Spread the love

MAAMBUKIZI mapya ya ugonjwa wa Malaria yamepungua nchini kwa asilimia 27 kutokana na kuboreka kwa takwimu ya ugonjwa huo ukilinganisha na kesi 164 mwaka 2015 hadi kesi 119 mwaka 2018. Anaripoti Mwandishi wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Leonard Subi, Mkurugenzi wa Kinga ametoa kauli hiyo leo tarehe 5 Januari 2020 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa umoja wa wabunge wa kupambana na malaria na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Tanzania (TAPAMA) na Alma (African Leaders Malaria Alliance).

Dk. Subi amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na jitahada za viongozi na muhimili wa Bunge katika ushirikiano wa kupambana na ugonjwa huo.

Amesema kuwa viongozi wa nchi za afrika wanapambania afya za wananchi na hivyo kwa Tanzania vifo vitokanavyo na Malaria vimepungua  kwa asilimia 63 kutoka vifo 6737 mwaka 2015  hadi 2,540 mwaka 2018.

“Ingawa hivi sasa tupo kwenye kudhibiti ila sasa hivi tuna lengo la kutokomeza,hivyo tuna imani kwamba tanzania tunao uwezo mkubwa wa kufikia huko kwani kuanzia Rais hadi muhimili wa Bunge nao wako mstari wa mbele kuondosha malaria nchini”.

Aidha, amesema kuwa hivi sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini kwa kupungua kwa wagonjwa wanaougua malaria kupungua pia hata kwa watoto chini ya miaka mitano wamepungua.

“Tanzania inapambana na wadudu dhurifu kuanzia ngazi ya viluilui hadi mbu wapevu,hivyo kila mwananchi anachukua hatua,hivyo ni vyema tukaungana ili kuiondosha Malaria nchini”.Amesema Dk. Subi

Naye Katibu wa TAPAMA Raphael Chegeni amesema msingi wa taifa ni kuwa na afya ,hivyo wanafarijika na afua zinazochukuliwa na wizara ya afya katika kupambana na malaria nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!