December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif: Zanzibar imetumbukizwa gizani

Spread the love

MKATABA  uliosainiwa Tarehe 23 Oktoba mwaka 2018 wa uchimbaji mafuta visiwani Zanzibar umetabiriwa kuwa ni chanzo kingeni cha Mgogoro ndani ndani ya Muungano wa Tanzania. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo terehe 11 Novemba 2018, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi amesema kuwa kusaiwa kwa mkataba huo kulikokiuka Katiba na sheria kutasababisha mgogoro ndani ya Muungano.

Maalim Seif amesema kuwa  Mkataba huo haujazingatia haki za Wazanzibar na umekwenda kinyume na Katiba na Sheria.

“Madhumuni makubwa ya Taarifa hii ni kuwatanabahisha Wazanzibari na Watanzania kwa jumla kwamba kwa kusainiwa Mkataba tulioutaja katika mazingira yaliyokosa umakini, yaliyojaa kutokujali Katiba wala sheria na maslahi mapana ya nchi na yenye utatanishi mkubwa na wa wazi wa kikatiba, kisheria na kisiasa, Zanzibar pamoja na vizazi vijavyo inaingizwa katika janga kubwa sana,” amesema Maalim Seif.

Mkataba huo ulisainiwa na Serikali ya Zanzibar na Kampuni ya Utafutaji na Uchimbaji Mafuta ya Rak Gas kutoka katika nchi ya Ras Alkhaimah ya taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu [United Arab Emirates-UAE].

Mkataba uliotiwa saini ni kwa ajili ya kugawana faida itayopatikana pindipo uchimbaji wa mafuta au gesi utafanyika katika kitalu cha Zanzibar-Pemba [Production Sharing Agreement- PSA].

Amesema kuwa Suala la rasilimali ya mafuta na Gesi lina umuhimu wa aina ya pekee kwa Zanzibar na watu wake kutokana na mazingira ya kikatiba, kisheria na kiuchumi

“Serikali imesaini mkataba wa uchimbaji  Bila ya kuwepo umakini, ukweli wa dhati wa wanaolisimamia na uwazi, Zanzibar, watu wake na vizazi vyao vya baadae watajikuta wameingizwa katika mgogoro mwengine mkubwa sana sawa au zaidi ya ule mgogoro wa Mkataba wa Muungano,” ameeleza Maalim Seif.

Wakati huohuo amemtaka Rais John Magufuli kuingulia kati suala hilo kabla ya kuibuka kwa mgogoro kutokana na uhodali wake wa kuyatatua matatizo yanayoikabili nchi.

error: Content is protected !!