Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif, Shilungushela watoana jasho
Habari za Siasa

Maalim Seif, Shilungushela watoana jasho

Maalim Seif Shariff Hamad na Nyagaki Shilungushela wagombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo
Spread the love

MAALIM Seif Shariff Hamad, Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amechuana vikali na mwanasiasa nguli, Nyagaki Shilungushela katika mdahalo wa kupima wagombea wa uenyekiti wa chama hicho. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Wagombea hao wamechuana vikali kujibu maswali katika mdahalo huo, unaofanyika leo tarehe 13 Machi 2020, katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam unaondeshwa na Absalom Kibanda, Mwenyekiti Mstaafu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEC). Yeremia Maganja, aliyekuwa pia mgombea wa nafasi hiyo, hakutokea.

Akijinadi katika mdahalo huo, Maalim Seif amesema ameamua kugombea nafasi hiyo, akiamini kwamba kutokana na uzoefu wake katika siasa, kitakua imara na hata kuchukua dola katika Uchaguzi Mkuu wa mwala 2025.

“Natumaini kama nitachaguliwa kuwa kiongozi, nafasi ya uenyekiti nitakisaidia chama kutokana na uwezo wangu nilio nao. Nitatumia uzoefu wangu kukiimarisha chama.

“Katika miaka mitano kama nikichaguliwa nitahakikisha kitakua chama imara ili uchaguzi 2025 tuweze kuunda serikali au sehemu ya serikali Zanzibar. Hilo halina shaka, au kuwa na wabunge wengi na hata kuwa sehemu ya Serikali Tanzania,” amejinadi Maalim Seif.

Kwa upande wake Shilungushela Nyangaki, amejipambanua kama mwanasiasa asiyependa siasa za propaganda. Na kwamba anapenda siasa za uhalisia.

Amesema anataka kugombea ili kuleta mageuzi ya upinzani na kuacha siasa za kuondoa madarakani bila mikakati, bali kujenga chama imara chenye mizizi mizuri ya kungoa madarakani.

“Sifanyi siasa za propaganda. Ninaeleza kile cha ukweli. Kwa nini nimeamua kugombea, kwa sababu moja lakini la msingi Tanzania hakuna chama chenye maandiko, nitakufuru nikisema matakatifu lakini yaliyo bora kwa jamii ya Tanzania kama ACT Wazalendo, ndio maana nikashawishika. Yanaendana na uhalisia si propaganda,” amesema.

Shilungushela amejinadi kwamba, kama chama hicho kitampa nafasi, atahakikisha utendaji wake unaleta manufaa ndani ya chama hicho.

“Chama kama hiki nitakifanyia nini? Nyie vijana kama mnataka kurithi chama chenye msimamo na kitakubalika kwa mtu yoyote hebu fuata uongozi wangu,” amesema.

Kuhusu Maganja ambaye naye ameonesha nia ya kugombea uenyekiti wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, amesema hadi sasa hajafika kutokana na sababu zilizo nke ya uwezo wake.

Mdahalo huo ulianza majira ya saa tisa na nusu alasiri lakini hadi sasa Maganja hajawasili katika mdahalo huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!