Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: Safari hii tunakaba kote
Habari za Siasa

Maalim Seif: Safari hii tunakaba kote

Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo
Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema, kwenye Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, hakitaruhusu sehemu yoyote Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupita bila kupingwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho leo tarehe 3 Agosti 2020, katika Ukumbi wa Mikutano wa Lamada, Ilala jijini humo Maalim Seif amesema, yale mazoea ya CCM kupita kwenye majimbo na Kata sasa yatakoma.

Mbele ya wajumbe wa mkutano huo, Maalim Seif ambaye amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea urais visiwani Zanzibar amesema, wajumbe wa mkutano huo wana wajibu kuhakikisha kwenye mikoa na wilaya zao, hakuna kata wala jimbo litakaloingia kwenye uchaguzi huo bila chama hicho kusimamisha mgombea.

“Safari hii tunakaba kote, yale mazoea ya CCM kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi huu hayapo, nyinyi ndio mpo huko kwenye mikoa na wilaya zenu, hakikisheni kila eneo tumesimamisha mgombea,” amesema Maalim Seif na kuongeza:

          Soma zaidi:-

“Hiki ni kikao cha kazi na kazi inaanzia hapa, hatushiriki uchaguzi bali tunakwenda kushinda. Wajumbe wa halmashauri kuu wote tuonekane manahodha katika maeneo yetu. Wenyeviti wa mikoa, makatibu wa mikoa tusimame imara.”

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo akimkabidhi fomu ya kugombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad

Maalim seif amewataka wajumbe hao kwenda kufanya utafiti wa idadi ya kata zilizo kwenye maeneo yao na kuhakikisha mtu anayepitishwa, anakubalika.

“Tutakaporejea kwenye maeneo yetu, tuhakikishe kwanza kuna kata ngapi, na je una wagombea wangapi? Tuhakikishe hatuiachi CCM inapita bila kupingwa mahali popote pale.

“Ugonjwa ule wa nyinyi mnaanza moja, wao wanaanza 41 tuuache. Kusiwe na kata isiyo na mgombea. Tuna kazi nzito kwenye uchaguzi huu na kazi yenyewe inaanzia leo,” amesema.

Benard Membe (kulia) akiwa na Maalim Seif

Kikao cha Halmashauri Kuu kinafanyika leo ikiwa ni baada ya kutanguliwa na kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jana tarehe 2 Agosti 2020.

Kwenye kikao cha leo, wajumbe wa mkutano huo watapitisha jina la mgombea urais wa Tanzania Bara na Visiwani. Majina yanayotarajiwa kupitishwa ni la Bernard Membe aliyeomba kuteuliwa kugombea urais Tanzania Bara na Malim Seif aliyeomba kugombea urais visiwani Zanzibar.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!