August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif pasua kichwa

Spread the love

SERIKALI ya Dk. Ali Mohammed Shein haipati usingizi. Ni kutokana na Maalim Seif Shariff Hamad kuumiza vichwa vyao, anaandika Hamisi Mguta.

Jeshi la Polisi visiwani humo leo limemuhoji Maalim Seif, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF) takriban kwa saa tatu. Hata hivyo limemwacha.

Tangu kumalizikwa kwa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana na matokeo yake kuvurugwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa maslahi ya Dk. Shein ambaye ni mgombea wa CCM, Maalim Seif amekuwa mwiba visiwani humo.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya jeshi hilo, mahojiano hayo yalihusu tuhuma kwamba, ametenda kosa la uchochezi katika ziara aliyoifanya kisiwani Pemba katikati ya mwezi huu.

Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF anayepigania kurudishiwa haki yake ya ushindi wa urais katika uchaguzi mwaka jana, mara tu alipotoka Makao Makuu ya Polisi Ziwani mjini Zanzibar, alianza msafara wa kwenda Wilaya ya Kusini ambako awali alitarajiwa kuwasili asubuhi kuendelea na ziara ya kikazi ya kuhamasisha mkakati wa wananchi kudai haki yao ya kidemokrasia.

Ofisa mwandamizi wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai visiwani humo amesema, mahojiano hayakuwa rahisi.

Amesema, Maalim Seif mwenyewe alionekana imara na mchangamfu muda wote “lakini alionesha hasira alipohisi anaulizwa maswali ya mzaha, ” amesema.

Salim Bimani, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa CUF ameuamibia mtandao wa MwanaHALISI Online mchana huu kuwa, Maalim Seif aliandamana na jopo la mawakili watatu.

Miongoni mwao ni wakili maarufu visiwani humo, Awadh Ali Said ambaye alikuwa Kamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Mstaafu, Joseph Warioba

Baraza Kuu la Uongozi la CUF limeazimia chama kichukuwe hatua za amani kudai kukabidhiwa ushindi wake wa uchaguzi ambao ulihujumiwa wa hatua ya Jecha kutangaza 28 Oktoba 2015 kuufuta uchaguzi mzima kwa madai kuwa, uliharibika.

Chini ya shinikizo za CCM Jecha alilazimisha uchaguzi alouitwa wa marudio ambao ulifanyika 20 Machi 2016 na kumtangaza Dk. Shein mshindi kwa asilimia 91. CUF na vyama kadhaa walisusia uchaguzi huo.
Kuhusu hatua ya CUF katika kilichofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya Kiongozi wa chama hicho? Bimani amesema, wanajua yote hayo ni kutimiza matakwa binafsi ya CCM.

“Hawa CCM wanajua wanaongoza bila ya ridhaa ya Wazanzibari na wanadhani kumdhalilisha Maalim Seif kutaogopesha wananchi katika kudai haki yao,” amesema.

Amesema, Maalim Seif alishinda uchaguzi na kwamba, dunia yote inajua lakini kutokana na utamaduni wa ovyo kwa wakuu wa CCM wa kutoheshimu misingi ya demokransia na kutojali haki za Wazanzibari, walifanya mapinduzi ya uamuzi wa wananchi kwa kumtumia Jecha, Mwenyekiti wa ZEC.

Baraza Kuu la Uongozi la CUF limeazimia chama kichukuwe hatua za amani kudai kukabidhiwa ushindi wake wa uchaguzi ambao ulihujumiwa wa hatua ya Jecha kutangaza 28 Oktoba 2015 kuufuta uchaguzi mzima kwa madai kuwa uliharibika.

 

error: Content is protected !!