Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: Membe unaogopwa, gombea urais Tanzania
Habari za Siasa

Maalim Seif: Membe unaogopwa, gombea urais Tanzania

Bernard Membe (kulia) akiwa na Maalim Seif Sharrif Hamad
Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema, Bernard Membe anaogopwa. Anaandika Yusuph Katimba..(endelea).

Membe amejiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kufukuzwa uanachama kwa madai ya utovu wa nidhamu

Akizungumza muda mfupu baada ya Membe ambaye ni Waziri wa Mamboo ya nje wa zamani kuzungumza na wanachama wa chama hicho leo Alhamisi tarehe 16 Julai 2020 katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam, Maalim Seif amesema, ACT-Wazalendo imeokota kitu chenye thamani (Membe).

“Tumevuna, nina hakika chama hiki kitapaa. Mimi na wenzangu tulipojiunga tulianzisha awamu ya kwanza ya shusha tanga pandisha tanga, Membe anaanzisha awamu ya pili,” amesema Maalim Seif huku akishangiliwa

“Membe wanampenda wengi. Wanamfahamu uwezo wake, ujuzi wake na wanamfahamu uadilifu wake, wengi watamfuata. Membe ni maarufu na ndio maana wanamuogopa,” amesema

Maalim Seif amemsifu Membe kwamba ni mvumilivu na jasiri akisisitiza, chama hicho kama kilikuwa kikijulikana Kenya na Tanzania, sasa kitajukiana

Maalim Seif, M/kiti ACT-Wazalendo Taifa

“Membd ni maarufu, Membe amekuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka 10, kaijengea heshima Tanzania nje. Linganisha Tanzania ya Kikwete na Tanzania ya sasa, Membe amefanya kazi kubwa,” amesema Maalim Seifa.

Pia, amemsifu Membe kwa kuweka uhusiano mzuri kati ya Tanzania na mataifa ya nje

“Dunia inamtambua Membe, ana mahusiano na wakubwa wa nchi karibu zito duniani, ndio maana wanamuogopa, wanamjua uwezo wake, wanajua vipi anakubalika kimataifa,” amesema.

Maalim Seif amesema, alitumia fursa hiyo kumweleza kuwa wanachama wa chama hicho, wamemtuma aseme kwamba, Membe achukue fomu ya kuwania urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

Maalim Seif akiongozana na Benard Membe wakiingia ukumbini Mlimani City

Kauli hiyo iliibua shangwe kwa viongozi na wanachama waliokuwa ukumbini.

Hata hivyo, Membe aliyewahi kuwa mbunge wa Mtama Mkoa wa Lindi, hakuzungumzia lolote juu ya kauli hiyo ya Maalim Seif ya kumtaka kugombea urais.

Tayari Maalim Seif amekwisha chukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho ili agombee urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!