Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif kurejea tena Ikulu leo
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif kurejea tena Ikulu leo

Maalim Seif Sharrif Hamad, aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa
Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi leo Jumanne tarehe 8 Desemba 2020, atamwapisha Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Rais Mwinyi anamwapisha Maalim Seif ambaye ni Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo baada ya kuwa amemteua katika nafasi hiyo juzi Jumapili tarehe 6 Desemba 2020 kwa kutumia matakwa ya Kifungu cha 9(3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Kifungu hicho kinasema “Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakuwa na Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia.”

Rais Mwinyi alifanya uteuzi huo, ikiwa ni saa chache kupita siku hiyo tangu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutoa maazimio ya kikao cha kamati kuu kilichojadili suala hilo la kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Kikao hicho, kilikubali kwenda kushiriki katika Serikali hiyo pamoja na madiwani, wabunge na wawakilishi walioshinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 27 na 28 Oktoba 2020, kwenda katika vyombo vya uwakilishi kuanza majukumu yao.

Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo Zanzibar

Maalim Seif aliyezaliwa 22 Oktoba 1943, anarejea tena kwenye nafasi hiyo kwa mara ya pili baada ya ile ya mwaka 2010-2015 kuhudumu akiwa Chama Cha Wananchi (CUF) na Rais wa wakati huo alikuwa Dk. Ali Mohamed Shein.

Mbali na uteuzi huo wa Maalim Seif aliyekuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Rais Mwinyi amewateua pia viongozi wawili wa ACT-Wazalendo kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Walioteuliwa ni; Mwanasheria Mkuu wa ACT-Wazalendo, Omar Said Shaaban na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho-Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!