August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif kufunguka tena Marekani 

Spread the love

MAALIM Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi- CUF anatarajia kuzungumza na watanzania waishio mji wa Boston nchini Marekani,  anaandika Pendo Omary.

Mkuatano huo ambao utafanyika katika eneo la 42 Charles Boston umeandaliwa na Jumuiya ya Wanzanzibar waishio nchini humo. 

Pamoja na mambo mengine lakini suala la hali halisi ya kisiasa Zanzibar tangu kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba mwaka jana visiwani humo, linatazamiwa kuwa sehemu ya ajenda muhimu za mkutano huo.

Tangu kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi huo Seif amefanya jitihanda mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kile anachokiita kutafuta muafaka wa mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Moja ya jitihada hizo ni kufungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mjini The Hague kuhusu ukandamizaji na ukiukwaji haki za binadamu uliofanyika kabla na baada ya uchaguzi mkuu visiwani Zanzibar.

Seif yupo nchini Marekani kwa siku kadhaa baada ya kupata mwaliko wa kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na chama cha Democratic wiki iliyopita ambao ulimpitisha Bi. Hillary Clinton kuwa mgombea Urais wa chama hicho katika taifa hilo lenye nguvu zaidi kiuchumi duniani.

 

error: Content is protected !!