Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: Hiki ndicho kilichowaponza UAMSHO
Habari za Siasa

Maalim Seif: Hiki ndicho kilichowaponza UAMSHO

Spread the love

SIASA za kukomoana zimetamalaki Zanzibar na hiki ndicho kilichosababisha viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar kusota rumande bila sababu za kueleweka. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Zanzibar … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa na Maalim Seif Shariff Hamad, mshauri mkuu wa Chama ACT Wazalendo katika kongamano la kuadhimisha miaka tisa ya kuasisiwa kwa mfumo wa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK) lililofanyika tarehe 31 Julai 2019.

“Kitendo cha Masheikh wa Uamsho kuendelea kusota rumande jijini Dar es salaam kwa miaka sita bila sababu ya msingi, ni matokeo ya siasa za kukomoana zilizotamalaki Zanzibar baada ya kuhujumiwa kwa maridhiano ya Wazanzibari,” amesema Maalim Seif.

Viongozi wa Uamsho walikamatwa mwaka 2012 visiwani Zanzibar kwa madai ya kusababisha vurugu na kuhifadhi magaidi.

Akifafanua zaidi athari zinazotokana na kuvunjwa kwa maridhiano hayo, Maalim Seif alisema, baadhi ya jamaa, ndugu na hata marafiki wa viongozi hoa wamekuwa wakitishwa.

Ni wale ambao wamekuwa wakifuatilia taarifa na mwenendo wa suala la viongozi hao wa dini na maarufu visiwani humo.

Tarehe 31 Julai 2010, Wazanzibari kupitia kura ya maoni, zaidi ya asilimia 60 ya Wazanzibari walichagua kuongozwa kwa mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Kwa mara ya kwanza iliundwa baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010 na kuongozwa na Dk. Ali Mohammed Shein ambapo Maalim Seif akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Maalim Seif akiwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), kukutana kwa faragha na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na kukubaliana kufuta siasa chafu za ubaguzi chuki na uhasama. Mkutano wao ulifikia kilele tarehe 5 Novemba 2009.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!