January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif: CCM dubwasha lililoota mizizi

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad akihutubia katika Mkutano Mkuu wa Chadema

Spread the love

MAKAMU wa Rais Zanzibar Maalim Seif amewataka wananchi wapenda mabadiliko waungane pamoja katika kufanya kazi ya kukingoa Chama Cha Mapinduzi madarakani na kukifananisha dubwasha lililoota mizizi. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi (CUF), na mgombea pekee wa urais kwa kupitia tiketi ya Umoja wa katiba ya wananchi (Ukawa),Zanzibar amekipongeza Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kumpokea Edward Lowassa na kumteua kuwa mgombea urais.

Aidha, Seif ameyasema hayo leo katika Mkutano mkuu wa Chadema, ambapo pia amempongeza Lowassa kwa maamuzi magumu aliyoyafanya kwa kujiunga na Chadema na kukubali kuipeperusha bendera ya Ukawa kwa lengo la kuiondoa CCM madarakani oktoba 25 mwaka huu.

Katika mkutano huo walihudhuria wenyeviti wenza wa Ukawa ambao kwa pamoja walionekana kumuunga mkono Lowassa na kumpa baraka tele katika mapambano aliyoyaanzisha.

Wakitoa salamu mbalimbali kutoka katika vyama vyao, Mwenyekiti wa Chama cha NLD Dk.Emanueli Makaidi ambaye alionekana kumuunga mkono Lowassa kwa asilimia zote na kusema, “Chadema mmetuletea mkombozi wa taifa letu”.amesema.

Makaidi amewasihi wananchi kutohofia dola kushikwa na chama kingine kwa Chama Cha Mapinduzi kimepoteza zifa zake hivyo wananchi hawana budi kukihama bila hofu kwani inawezekana kuishi bila CCM.

“Mimi tangu nazaliwa sijawahi kujiunga na CCM wala kuteteleka mbona sijafa wala kuumwa? Sasa kwanini wananchi waogope kutoka CCM? Inabidi mfike sehemu muwe na maamuzi magumu kama ya Lowassa.na jua wapo wengi wnatamani ila wanaogopa”. Amesema Dk. Makaidi.

Hata hivyo amewataka Ukawa kutowazuia wanachama wapya wanaotaka kujiunga kwani umoja wao ndio utaweza kuiondoa CCM madarakani.” Njia ya matumaini ya Lowassa sasa inaenda kuwa safari ya uhakika,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia wakati akitoa salamu kutoka katika chama chake amesema, “kwanza nianze kwa kumpongeza Mwenyekiti taifa Chadema Freeman Mbowe kwa kukipigania chama na kukifikisha hapa kilipo.”

Mbatia pia amempongeza Lowassa kwa maamuzi yake ya kujiunga na Chadema na kusema, “watu wanamajungu sana na kitendo alichofanya lowasa hata mtume amewahi kufanya alipoona anapokaa kuna majungu mengi akahama, hivyo kwa kitendo hicho anatakiwa kupata thawabu”.

Ameongeza kuwa, kazi ya kuiondoa CCM madarakani ni kubwa ambayo inahitaji ushirikiano wa hali ya juu ili kuing’oa madarakani mwaka huu.

Mbatia amesema, “nawaomba vyombo vya dora kusimamia misingi ya haki za binadamu kwani nchi hii si ya CCM bali ni yetu wote”.

Mbatia amevisihi vyama vya Ukawa kuungana na kumsaidia Lowassa katika kupata wabunge bora na viongozi bora kutoka katika umoja huo.”umoja wetu ndio ushindi wetu”.Amesema Mbatia.

error: Content is protected !!