Wednesday , 6 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif azungumzia ‘usaliti’ kwa Rais Aboud Jumbe
Habari za Siasa

Maalim Seif azungumzia ‘usaliti’ kwa Rais Aboud Jumbe

Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi
Spread the love

WATU waliokuwa karibu na Rais Aboud Jumbe wakati huo, ndio walioiba waraka na kutoa nakala, kisha ule asili ‘original’ wakaurudishwa, nakala nyingine waliipeleka kwa Malimu (Mwal. Julius Nyerere). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Ni kauli ya Maalim Seif Sharif Hamad, aliyoitoa leo tarehe 15 Novemba 2019, akizungumzia tuhuma za kumfitinisha Rais Jumbe, aliyekuwa Rais wa Zanzibar kwa Mwal. Nyerere.

Akizungumza kwenye mahojiano katika kipindi cha Konani, kilichorushwa na Televisheni ya Mtandaoni ya ITV, Maalim Seif amesema, asingeweza kumsaliti Rais Jumbe kutokana na mchango wake kwake.

“Mimi kwamba inasemekana nilimfitini Abdu Jumbe, hapana si kweli, mimi Jumbe siwezi kumfitini. Yeye ndiyo alinifikisha nilipofika, kwa sababu nimekuwa waziri kwa sababu yake, mimi si mtu wa aina hiyo, kwamba huyu mtu alinifadhili halafu nimgeuke,” amesema Maalim Seif.

Maalim Seif amesema, usaliti ulifanywa na watu wa karibu wa Rais Jumbe ambao hakutaja majina yao, walimsaliti kwa kumuibia waraka kuhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kisha wakaupeleka kwa Mwalimu Nyerere.

Mwanasiasa huyo nguli wa Zanzibar ambaye sasa ni mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema, baada ya waraka huo kuibwa, ilionekana kwamba Serikali ya Zanzibar ina mpango wa kuuvunja muungano.

“Kabla ya kujiuzulu marehemu Jumbe, kulitokea kitu ambacho CCM walikiita kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa, ilikuwa Zanzibar wana madai yao.

“…kwamba lazima muungano huu utazamwe upya, suala hilo likaenda, ikaonekana kwamba serikali ya Zanzibar ina mpango wa kutaka kuvunja muungano,” amesema Maalim.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!