Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif kukinukisha
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif kukinukisha

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad amesema, amechoka kuchezewa. Amesema muda siyo mrefu atakinukisha. Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Zanzibar…(endelea).

Amesema, “wamenichezea kwa muda mrefu sana. Nasema, basi. Kama uvumilivu utakuwa umenifika mwisho. Sasa, wasubiri waone kitu nitachowafanyia mwaka huu.”

Maalim Seif alitoa kauli hiyo katika mkutano wake na Jumuia ya Wanawake ya chama hicho (JUKE- CUF), uliofanyika mwishoni mwa wiki Visiwani Zanzibar.

Mkutano ambao kiongozi huyo mashuhuri wa kisiasa Visiwani aliutumia kutoa kauli hiyo, ulifanyika katika Ukumbi wa Majidi, Kiembe Samaki nje kidogo ya Mji wa Unguja.

Amesema, “nimeambiwa kuwa wapo baadhi ya viongozi wa CCM hapa Zanzibar wanasema, nimekwisha na sina nafasi tena kwenye ulimwengu. Niwaeleze nipo makini na hakuna kiongozi yoyote wa CCM anaweza kunieleza chochote.

“Nawaambia hivi, bado nipo na nipo makini kabisa. Waendelee kufanya tu, lakini mwaka huu ndio watamjua vizuri Seif. Nitawafanyia kitu ambacho hawatakisahau katika maisha yao ya kisiasa.”

Maalim Seif amekuwa na mikutano mfululizo na jumuiya za chama hicho pamoja na viongozi wengine wa CUF ili “kujiandaa kwa lolote litakalotokea siku chache zijazo.”

CUF ipo katika mgogoro wa uongozi kufuatia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francies Mutungi, kuamua kinyume na sheria, kumrejesha kwenye chama hicho aliyekuwa mwenyekiti wake, Prof. Ibrahim Lipumba.

Prof. Lipumba alijiuzulu kwa hairia yake uenyekiti wa chama hicho, katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015 na baadaye kutokomea kusikokujulikana.

Kufuatia uamuzi huo, baadhi ya viongozi wa CUF wanamuunga mkono Maalim Seif, walilazimika kufungua kesi mahakamani kupoinga hatua hiyo.

Kwa mujibu wa rekodi zilizopo mahakamani, baadhi ya kesi hizo, uamuzi wake unatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi huu.

Maalim ameeleza wajumbe wa mkutano huo wa wanawake kuwa anakusudia kuwafundisha siasa kuanzia kwa Rais wa Jmhuri, John Magufuli hadi Dk. Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar.

Naye mwenyekiti wa JUKE-CUF, Fatma Fereji, amemuhakikishia Maalim Seif kuunga mkono uamuzi wowote watakaoufanya kwa maslahi ya Zanzibar na wanachama waaminifu wa chama hicho.

Alisema, “mimi kwa niaba ya wenzangu, tunakuunga mkono na kukuhakikishia kuwa tuko wote kwa lolote utakaloliamua. Wanawake wa CUF hawatorudi nyuma na kwamba kila unachotuletea, ndio tutakachokipokea.”

Fatma amesema, “Maalim, sisi haturudi nyuma. Wanawake wa CUF, siyo hulka yao kukata tamaa. Tutakuwa nawe bega kwa bega.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!