Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif aripoti ofisini kwake, atoa maagizo
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif aripoti ofisini kwake, atoa maagizo

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, amewataka watumishi wa ofisi yake, wanakuwa nadhifu kuanzia mavazi mpaka maeneo yao ya kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Amesema hayo leo Jumatatu tarehe 11 Januari 2021 mara baada ya kuripoti katika ofisi yake iliyopo Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Maalim Seif amepokelewa na watendaji wa ofisi hiyo, wakiongozwa na Kaimu Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais, Dk. Khalid Salum Mohammed.

Maalim Seif ameripoti ofisini ikiwa ni siku 34 zimepita tangu, Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi alipomwapisha kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, tarehe 8 Desemba 2020.

Akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali zilizopo chini ya ofisi yake, Maalim Seif amesema, ofisi hiyo ni miongoni mwa ofisi kubwa katika Serikali na muonekano wake pamoja na utendaji mzuri wa kazi unatakiwa kuwa mfano bora.

”Suala la nidhamu ni suala muhimu sana kwani bila nidhamu hatuwezi kufanya mambo yetu tukapata mafanikio. Wakuu wa idara, musimuonee mtu muhali katika hili na kama mtu asipokuwa na nidhamu aadhibiwe kwa mujibu wa sheria ila nasisitiza zaidi asionewe mtu,’’ amesema Maalim Seif.

Amesema, suala la ushirikiano ni miongoni mwa mambo muhimu na “ushirikiano huu uwepo kwa mtu mmoja mmoja lakini pia kwa taasisi kwa ujumla.”

Maalim Seif ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo, katika kusisitiza hilo, amesema yeye anawakaribisha watendaji wote katika ofisi yake kwa ushauri na ufafanuzi kwa maslahi mapana ya taasisi na Taifa kwa ujumla

Pia, amewataka watendaji hao kujiwekea malengo kama kwani ”tunahitaji tukamilishe majukumu yetu yote yanayotupasa kufanya tena kwa ufanisi mkubwa na hili litafanikiwa kama tutajiwekea malengo katika utendaji wetu.”

“Niwaombe wakuu wa idara na watendaji wote muwe na mikakati ya malengo yetu ya muda mfupi na ya muda mrefu ili kuhakikisha hakuna kitu tutakachokiwacha nyuma,’’ amesema

Amewaeleza, ataanza ziara rasmi ya kupitia idara hizo kuanzia Jumaatano hii ili kujua changamoto na kubadilishana mawazo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!