Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif aongeza joto la siasa Z’bar
Habari za Siasa

Maalim Seif aongeza joto la siasa Z’bar

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo akimkabidhi fomu ya kugombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad
Spread the love

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiendelea na mchujo wake kwa watia nia wa urais visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad tayari amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo visiwani humo. Anaripoti Mwamdishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Maalim Seif amechukua hatua hiyo ikiwa ni siku saba baada ya kutangaza nia ya kuwania urais visiwani Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.

Maalim Seif ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo na Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Wananchi (CUF), amechukua fomu hiyo leo tarehe 5 Julai 2020 katika ofisi za chama hicho zilizopo Vuga, Zanzibar.

          Soma zaidi:-

Akionesha tabasamu, Maalim Seif amekabidhiwa fomu hiyo kutoka kwa Ado Shaibu, katibu mkuu wa chama hicho. Mwanasiasa huyo mkongwe visiwani Zanzibar amesindikizwa na viongozi mbalimbali akiwemo Salim Biman, Katibu wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho.

Tarehe 28 Juni 202, mbele ya wanahabari visiwani humo Maalim Seif alitaja mambo matano yaliomsukuma kufikua uamuzi wa kuwania urais visiwani humo kwa mara ya sita.

Sababu hizo alisema ni:-

Kwanza; hata kabla ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, yeye na wenzake hawakuridhishwa na namna visiwa hivyo (Unguja na Pemba) vilivyokuwa vikiendeshwa.

“Mimi na wenzangu kadhaa tulikuwa haturidhishwi na jinsi nchi yetu inavyoendeshwa. Kwa pamoja tulianzisha vuguvugu au movement ya kuweka shinikizo kwa dola kuruhusi mfumo wa vyama vingi,” alisema.

Pili; Maalim Seif alisema, mwaka 1992 walizanisha Chama cha Wananchi (CUF), kwa malengo ya wazi ya kurejesha haki za Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla ambazo mpaka sasa hazijarejeshwa.

“…lakini serikali ikaamua kutumia dola na taasisi zake na hasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na mahakama, kuingilia chama kile na kukidhoofisha kwa kukikabidhi kwa vibaraka wao ambao walipewa kazi ya kutufukuza uanachama mimi na wenzangu.

Tatu: alisema, amekuwa akiaminiwa kwa kiwango kikubwa na Wazanzibar katika kila chaguzi alipogombea, hivyo si vyema kupuuza imani hiyo.

“Viongozi na wanachama wenzangu waliniamini na kunipa bendera ya chama cha awali mwaka 1995, 2000, 2005 na 2015. Katika chaguzi zote hizo, Wazanzibar walinipa imani zao, na kila uchaguzi kura ziliongezeka.

“Nimeona si uungwana hata kidogo kudharu imani hiyo isiyokwisha kwangu, na amabayo imekuwa ikiongezeka kadiri siku zinavyokwenda, na badala yake ninapaswa kuihshimu,” alisema.

Nne: alisema kwamba, nguvu za giza za watawala zilitumika kupunguza nguvu ya wananchi, pia kulazimisha wagombea wa CCM kutangawa washindi licha ya kukataliwa na Wazanzibari.

“Nimeona kuwa, wakati umefika kwa nguvu hizo za giza za watawala kutambua kuwa, nguvu ya umma inapoamua kamwe haiwezi kushindwa, na kwamba uchaguzi huu tutaulinda ushindi wetu katika hali yoyote ile,” alisema.

Tano: Maalim Seifa alisema, uchaguzi mkuu 2015, ilikuwa ni tokeo la kubadilisha historia Zanzibar kwa maana Wazanzibari wengi walikataa kuongozwa na CCM.

“…lakini serikali haikujali kwa CCM kwamba imeishapoteza imani kwa Wazanzibar, ilimtumia Jecha (Salim Jecha, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar) kupindua matokeo.

“Nimeamua kutaka kuwapa kile walichokitaka mwaka 2015, wadhihirishe tena chaguo lao la mwaka 2015 na kuionesha dunia kuwa, maamuzi ya wananchi ni yale yale,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!