October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif aonesha njia ya ushindi 2020

Maalim Seif Shariff Hamad

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema, ushirikiano ndio njia muhimu ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Kutokana na hali hiyo amesema, ACT-Wazalendo wanahitaji ushirikiano na vyama vingine vya upinzani ili kukishinda Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Msimamo wa ACT-Wazalendo, tunaamini tunahitaji mashirikiano, hatuwezi kwenda kwenye uchaguzi huu chama kimoja kimoja.

“Mwaka 2015 kuna maeneo tulipoteza kwa kura chache, kwa kuwa kura ziligawika, wapinzani wangeungana CCM ingepoteza. Vyama vilivyo serious (makini) kuungana na kushirikiana ni jambo muhimu sana sana, tunahitaji kufanya kazi pamoja,” amesema Maalim Seif.

Amesema, tayari chama chao kimeanza taratibu kuhakikisha kunakuwa na ushirikiano kwenye uchaguzi huo, “ni mapema mno kusema tumefikia hatua gani, lakini response (mwitikio) tuliyoipata sio mbaya.”

Amesema, wananchi wana imani naye na kwa bahati nzuri kila uchaguzi kura zake zimekuwa zikiongezeka kwa kuwa anaaminiwa na Wazanzibari.

“Mimi ni mwanasiasa, kubwa wananchi wana imani name. Mara zote nagombea niliamini wananchi wana imani na mimi ndio maana ninashinda.

“Wakati wwt nitapoona imani ya wananchi imepotea, sintoendelea lakini sasa hivi kwa uchunguzi wetu, bado wananchi wana imani na mimi na sasa wanasubiri maamuzi yangu,” amesema.

error: Content is protected !!