Tuesday , 3 October 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif aondoka na ‘kijiji’ CUF
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif aondoka na ‘kijiji’ CUF

Maalim Seif Shariff Hamad
Spread the love

HATUA ya Maalim Seif Shariff Hamad kundoka katika Chama cha Wananchi (CUF) na kuhamia Chama cha ATC-Wazalendo imeathiri chama chake cha awali. Anaripoti Bupe Mwakiteleko …(endelea).

Maeneo mbalimbali nchini yaliyokuwa na ofisi za matawi ya CUF pamoja na viongozi wao leo tarehe 19 Machi 2019 wanatarajiwa kuhamia chama cha ACT-Wazalendo ikiwa ni siku moja baada ya Maalim Seif kuimwaga CUF.

Tayari Rashid Jumbe, Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Tanga ametoa maagizo kwamba, ofisi za wilaya na kata zote 27 zilizopo kwenye wilaya yake zishushe bendera za CUF na kupandisha za bendera za ACT-Wazalendo.

Pamoja na maagizo hayo Jumbe amesema, leo ndio kutakuwa na kazi rasmi ya kubadilisha kila kilichokuwa kikitumika na CUF sasa kutumika kwa niaba ya ACT-Wazalendo zoezi litalokwenda sambamba na kukabishi uanachama na kadi za chama walichohamia.

“Ofisi zote za CUF sasa zitapandishwa bendera za ACT-Wazalendo,” amesema Jumbe na kuongeza; “viongozi na wanachama wote wa CUF watajiunga na kupatiwa kadi za chama cha ACT-Wazalendo. Hivi ndivyo tulivyoamua.

Jumbe ameeleza kuwa, waliokuwa viongozi wa CUF baada ya kukabidhia kadi ya uanachama wa ACT-Wazalendo, watafanya kazi ya kupokea wanachama wapya ambao wapo tayari kwenda sambamba na mabadiliko makubwa yanayotarajiwa.

Kabla ya jumbe kutoa kauli ya yeye na viongozi wa wilaya hiyo kuhamia ACT-Wazalendo, kilichotangulia ni baadhi ya wanachama wa CUF kuendesha zoezi la kuchoma bendera ya chama hicho kuonesha kumpinga Prof. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa CUF na wale wanaomkubali.

Huko Zanzibar mambo yamezidi kuyumba kwa CUF ambapo sasa Makao Makuu ya chama hicho yamefungwa rasmi huku ndani kukiwa kumetolewa kila kitu. Licha ya kufungwa, tayari bendera za CUF zimeshushwa.

Kumekuwepo na makundi mbalimbali yakiendesha mjadala kuhusu hatua ya Maalim Seif kuhamia ACT-Wazalendo huku wakionesha kuridhishwa na uamuzi huo.

“Katika siku niliyofurahi kwenye siasa za Tanzania basi ni leo (jana), nimefurahi sana baada ya Maalim Seif kuhama chama na kukiacha chama kilichotekwa na CCM na serikali yake.

“CCM na serikali yake ndiyo walioharibu chama hiki, imekichukua kutoka kwa wana CUF na kwenda kumkabidhi Lipumba, sasa kama chama ni Lipumba tumeamua kumwachia. Wazanzibari tunakwenda kule alipo Maalim Seif,” amesema Ami Rashid Maalim, aliyekuwa mwanachama wa CUF.

Viongozi wengine kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wanatarajiwa kutoa misimamo yao leo kutokana na mgogoro uliodumu kwenye chama hicho kwa miaka mine sasa na hatua ya Maalim Seif kuhamia ACT-Wazalendo.

Akiondoka CUF Maalim Seif amesema, pamoja na kuamua kulitumia jukwaa la ACT-Wazalendo bado wanaamini ushirikiano katika vyama vyote.

“Niwahakikishie kwamba, bado tunaamini katika ushirikiano wa vyama vyote makini vya siasa na makundi mengine ya kijamii katika mapambano yetu ya kuleta demokrasia na haki nchini,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bilioni 6.1 kumaliza tatizo la maji Katoro-Buseresere – Geita

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM, (UWT), Zainab Shomari...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kupokea ndege ya 14 ya ATCL, safari kuongezeka

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania, kesho tarehe 3 Oktoba 2023, inatarajia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mobhare Matinyi Msemaji mpya wa Serikali

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mkuu wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Basi la Magereza lagonga treni yenye abiria 650 Dar

Spread the loveBasi  Jeshi la Magereza lenye namba MT 0040 limegonga treni...

error: Content is protected !!