MAALIM Seif Sharif Hamad, Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, ‘amemvimbia’ Hamadi Massauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kwamba hawezi kumzuia kufanya siasa Visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo tarehe 13 Desemba 2019, siku moja baada ya Masauni kuagiza kushuswa vyeo Makamanda wa Jeshi la Polisi, Mikoa ya Kaskazini Pemba na Kusini Unguja.
Masauni aliagiza hivyo kwa madai, polisi hao wamefanya kosa la kumruhusu Maalim Seif afanye mikutano ya hadhara.
Akizungumzia hatua hiyo, Maalim Seif amesema, hakuna mtu wa kumzuia Zanzibar, na kwamba atakwenda popote atakapo.
“Nakwambia Masauni hakuna mtu wa kunizuia Zanzibar nitakwenda popote nitakapo ndani ya nchi yangu,” amesema Maalim Seif.
Makamanda walioshushwa cheo ni, Sheikhani Mohamedi Sheikhani, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba na Hassan Nassir Ally, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kusini Unguja.
Maalim Seif yuko Visiwani Zanzibar kwenye ziara ya kukusanya maoni ya wananchi, kwa ajili ya kuandaa ilani ya ACT-Wazalendo ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
Leave a comment