Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif ampiga ‘stop’ Prof. Lipumba
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif ampiga ‘stop’ Prof. Lipumba

Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF. Picha ndogo Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimethibitisha kuwa hakitashiriki uchaguzi mdogo wa marudio katika jimbo la Buyungu, mkoani Kigoma, Jang’ombe Unguja na kata 79 Tanzania Bara. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya umma ya chama hicho, Mbarala Maharagande, amaiambia MwanaHALISI Online kuwa CUF hakitashiriki chaguzi hizo kutokana na kupandikiziwa mgogoro.

Uchaguzi mdogo katika jimbo la Buyungu, mkoani Kigoma, unafaanyika kufuatia kufariki dunia kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Mwalimu Kasuku Bilago (CHADEMA). Mwalimu Bilago alifariki dunia, tarehe 26 Mei mwaka huu.

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja siku moja baada ya Magdalena Sakaya, naibu katibu mkuu anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa, kutangaza kuwa chama hicho kitashiriki uchaguzi huo.

Maharage ni afisa mtendaji wa CUF, anayemuunga mkono Maalim Seif Shariff Hamad, katibu mkuu wa chama hicho taifa.

Uchaguzi mdogo unafanyika katika halmashauri za Moshi, Ruangwa, Mbulu, Hanang, Babati, Serengeti, Tarime, Kyela, Mtwara, Newala, Kilombero, Kilosa, Kwimba, Makete, Wanging’ombe, Kalambo, Songea, Msalala, Meatu na Singida.

Nyingine, ni Songwe, Tunduma, Tabora, Nzega, Urambo, Tanga, Karatu, Longido, Arusha, Ngorongoro, Monduli, Meru, Ubungo, Kondoa, Mpwapwa, Chamwino, Iringa, Kyerwa, Misenyi, Muleba, Nsimbo, Kasulu na Same.

Kwa mujibu wa Maharagande, kamati tendaji ya ya CUF, taifa iliyokutana makao makuu ya chama hicho, Mtendeni Unguja, imefanya uchambuzi wa kina na tathmini pana juu ya taarifa ya kufanyika kwa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 12 Agosti 2018, katika kata 79 na majimbo ya Buyungu na Jang’ombe.

Anasema, “kamati kimeamua kutoshiriki uchaguzi huo kutokana na kuwapo mkanganyiko wa uongozi katika usimamizi wa uchaguzi unaofanyika, kufuatia kuibuka mgogoro uliopandikizwa ndani ya CUF na Lipumba na washirika wake.

Hivyo basi, tumeona ni busara kwa sasa, kuelekeza nguvu na rasilimali zetu chache zilizopo kwenye kushughulikia mgogoro huu uliopandikizwa na kuupatia ufumbuzi.”

Maharagande anasema, “the Civic United Front (CUF), kinatoa wito kwa vyama rafiki vyote kwenye UKAWA kukaa pamoja na kufikia muafaka na maridhiano ya kusimamisha wagombea bora, imara na madhubuti kwenye nafasi zote hizo.”

Aidha, Maharagande amewataka viongozi na wanachama wote wa CUF katika maeneo ambako kunafanyika uchaguzi wa marudio kushirikiana bega kwa bega na kuunganisha nguvu za pamoja na vyama rafiki vya UKAWA ili kusaidia “kukishinda Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vibaraka wake.”

Kwa mujibu wa Maharagande, katika kata 79 kulikotangazwa uchaguzi, chama chake kimepoteza kata 4 kutokana na madiwani wake kujiengua na kujiunga na CCM na mwingine kufariki dunia.

Kata ambazo madiwani wake walijiengua, mbili zipo manispaa ya Tanga na moja iko Mtwara Vijijini. Diwani aliyefariki anatokea wilayani Kwimba.

Kutokana na vigezo vya kitaalamu na kitakwimu – election strategies – pamoja na ramani ya maeneo utakapofanyika uchaguzi, naibu mkurugenzi anasema, “CUF kingeweza kushiriki kikamilifu katika kata za mkakati 11 pekee.”

Anasema, “kata zingine tungelazimika kuunganisha nNguvu na vyama vingine katika UKAWA. Huu ndio msimamo wa chama unaozingatia maslahi mapana ya CUF (taasisi) unaopaswa kuheshimiwa na kuzingatiwa na kila mwana-CUF wa kweli.”

Hata hivyo, kutokana na mazingira tuliyonayo, hatutaweza kushiriki uchaguzi huo.

Akizungumzia uchaguzi mdogo wa Jang’ombe, Unguja, Maharagande anasema, msimamo wake uko wazi; hakitashiriki uchaguzi huo.

Alisema, “msimamo wetu huu, unatokana na ukweli kwamba msingi wa uchaguzi huo unatokana na uchaguzi haramu wa 20 Machi 2016, ambao uliweka wajumbe wa baraza la wawakilishi haramu, madiwani haramu na serikali haramu.”

Anasema, “CUF kinawataka wananchi wake wote wapenda demokrasia ya kweli kutoshiriki kwa namna yoyote ile katika uchaguzi huo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!