May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif amjibu Dk. Mwinyi

Maalim Seif Sharrif Hamad, aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Spread the love

MAALIM Seif Shariff Hamad, aliyekuwa mgombea urais visiwani Zanzibar kupitia Chama cha ACT – Wazalendo, amesema ‘chama hakijaamua’ kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Mwanasiasa huyo nguli wa Zanzibar na mwenyekiti wa chama hicho amekiri kupokea barua ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kumtaka jina la Makamu wa Kwanza wa Rais visiwani humo kwa mujibu wa katika ya nchi hiyo.

“Chama hakijakaa na kuamua kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” amesema Maalim Seif siku moja baada ya Dk. Mwinyi kueleza kwamba, kwenye uteuzi wake wa Baraza la Mawaziri jana tarehe 19 Novemba 20202 , ameacha nafasi mbili kwa ajili ya kusubiri uamuzi wa Chama cha ACT-Wazalendo kuapisha wawakilishi wao na kisha kuwajumuisha kwenye serikali yake.

           Soma zaidi:-

Maalim Seif na chama chake cha ACT – Wazalendo waligomea matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, wakieleza kufanyiwa hujuma.

“Chama cha ACT – Wazalendo kina idadi ya viti vya uwakilishi waliochaguliwa, ndio maana nimeacha nafasi mbili endapo watakuwa tayari lakini ukweli ni kwamba, hadi leo hawajaenda kuapishwa, kwa hiyo hawajasajiliwa kwa hiyo lazima tuwape muda wa kikatiba, hiyo ndio sababu,” alisema Dk. Mwinyi.

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi

Kwenye matokeo ya uchaguzi huo, chama hicho kilipata zaidi ya silimia 10 ya kura zote na hivyo kuwa na sifa ya kujumuishwa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani humo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

“Chama bado kipo kwenye mashauriano, mashauriano hayo yapo poa kwa wale waliopewa ubunge, uwakilishi na udiwani,” amesema Maalim Seif.

Visiwani Zanzibar, ACT-Wazalendo kimepata jumla ya wawakilishi wanne na sasa wamebaki watatu baada ya Abubakar Khamis Bakary, aliyekuwa  mwakilishi mteule wa Pandani kufariki dunia.

error: Content is protected !!