Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif alivyoacha pigo ACT-Wazalendo, Zitto asema…
Habari za SiasaTangulizi

Maalim Seif alivyoacha pigo ACT-Wazalendo, Zitto asema…

Spread the love

 

KIFO cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, kilichotokea Jumatano tarehe 17 Februari 2021, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, kimeacha pigo ndani ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, katika maziko ya mwili wa Maalim Seif, yaliyoanyika tarehe 18 Februari 2021, kijijini kwao Nyali Mtambwe, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar.

Akizungumzia kifo cha Maalim Seif , Zitto amesema, ACT-Wazalendo imempoteza mtu muhimu kwa kuwa alikuwa mlezi na mshauri katika masuala ya kisiasa ya chama hicho.

Zitto amesema, Maalim Seif alikuwa mpatanishi katika vikao vya ACT-Wazalendo, na kwamba pale chama hicho kilipokaribia kukata tamaa kutokana na mazingira magumu ya kisiasa, alikuwa anawapa ujasiri.

“Kwetu sisi ACT-Wazalendo, tumempoteza mtu muhimu sana katika malezi ya kisiasa na mshauri wetu mahiri,” amesema

“Tumempoteza mshauri na mpatanishi kwenye vikao vya chama chetu na mtu aliyetupa ujasiri mkubwa wa kusonga mbele hata pale ambapo tulikaribia kukata tamaa kutokana na madhila na mazingira magumu ya kisiasa katika siku za hivi karibuni,” amesema Zitto.

Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo amesema, kila chama hicho kilipokata tamaa, kilitumia mapito magumu aliyokumbana nayo Maalim Seif katika harakati zake za siasa, kujipa moyo na ujasiri.

“Kila tulipokaribia kukata tamaa au kukatishwa tamaa, tumekuwa tukijikumbusha mapito magumu aliyoyapitia Maalim Seif katika mapambano ya kudai haki, heshima na ustawi wa wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla,” amesema Zitto.

Zitto amesema “kila tulipojikumbusha mapito ya Maalim Seif, tunajiona bado tunayo nguvu kubwa ya kusonga mbele zaidi katika mapambano ya kudai haki na ustawi wa wananchi wenzetu.”

Mwanasiasa huyo amesema, licha ya Maalim Seif kukutana na misukosuko katika mapambano ya kudai haki, aliendelea kusimama imara.

“Madhila yote aliyopitia, miaka yote aliyotumikia jela, kejeli zote alizofanyiwa, uongo wote aliozushiwa na hila zote alizofanyiwa, Maalim Seif, aliendelea kusimama imara na kutetea haki za wananchi. Hakika, Maalim alikuwa kioo na chetu kwenye kisiasa,” amesema Zitto.

Machi 2019, Maalim Seif akiwa na asilimia kubwa ya wafuasi wake, alijiunga na ACT-Wazalendo, chama kilichoanzishwa mwaka 2014 akitokea Chama cha Wananchi (CUF), na kwamba ujio wake huo ulikiwezesha chama hicho kuteka siasa za Visiwa vya Zanzibar.

Kabla ya ujio wa Maalim Seif ndani ya ACT-Wazalendo, chama hicho kilikuwa na nguvu Tanzania Bara.

Ambapo kilifanikiwa kupapata jimbo moja la Kigoma Mjini na kuongoza Halmashauri ya Kigoma Ujiji baada ya kupata madiwani wengi katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Miezi kadhaa baada ya kujiunga na ACT-Wazalendo, Maalim Seif alichaguliwa kuwa Mshauri Mkuu wa chama hicho hadi Januari 2020 alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, nafasi aliyohudumu hadi umauti ulipomkuta.

Ujio wa Maalim Seif ndani ACT-Wazalendo, ulikifanya chama hicho kupata wabunge wanne visiwani Zanzibar, pamoja na kushika nafasi ya pili kwa wingi wa kura za urais.

Maalim Seif aligombea Urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, akichuana vikali na aliyekuwa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Mwinyi, na kuambulia nafasi ya pili.

Matokeo hayo ya uchaguzi wa urais Zanzibar yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC), yalikipa nafasi ACT-Wazalendo kushiriki kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Deni la Serikali laongezeka kwa trilioni 11

Spread the loveDENI la Serikali imeongezeka kwa takribani Sh. 11 trilioni sawa...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Mapya yaibuka wamasai waliohamishwa Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the loveMAPYA yameibuka kuhusu zoezi la Serikali kuwahamisha kwa hiari wamasai...

Habari MchanganyikoTangulizi

Baba aomba msaada kuzika miili ya familia yake iliyofunga bila kula kuonana na Mungu

Spread the loveWAKATI Mamlaka nchini Kenya, ikiendelea kukabidhi miili ya watu waliofariki...

error: Content is protected !!