July 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif ‘alianzisha’ kwa Dk. Shein

Spread the love

HALI ya hewa visiwani Zanzibar haijatulia, vidonda vya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana vinaendelea kutafuna visiwa hivyo, anaandika Happiness Lidwino.

Maalim Seif Shariff Hamad, aliyekuwa mgombea urais visiwani humo kupitia Chama cha Wananchi (CUF) amezidi kulaani utawala wa Dk. Ali Mohammed Shein kwamba, anaongoza ‘viwiliwili vya Wazanzibar na si nyoyo zao.’

Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF amesema, Dk. Shein anajidanganya kuwa yeye ni Rais wa Zanzibar na kwamba, wananchi visiwani humo wanamtambua yeye (Maalim) kuwa rais wao.

“…anajidanganya tu huyo Dk. Ali Mohammed Shein. Hapa yeye si rais, wananchi walimchagua maalim na yeye ndiye wanayemtambua kuwa rais wao,” amesema Malim Seif.

Kiongozi huyo wa CUF ametoa kauli hiyo jana wakati wa ziara yake ya siku nne katika Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Ametoa msisitiza kwamba, Zanzibar haina serikali halali na yale yote yanayofanywa visiwani hapo kwa sasa yanafanywa na utawala haramu wa Dk. Shein.

Hata hivyo Maalim Seif amesema kwamba, CUF ipo kwenye mkakati wa kufungua mashitaka kwenye Mahakama ya Kimataifa na kuwa, kinachofanyika kwa sasa ni kukusanya ushahidi wa kila aina.

Maalim Seif amewataka viongozi wa chama hicho kuwa tayari kuendelea na msimamo wa chama hicho na kwamba, ambaye hayupo tayari basi arudishe kadi ya chama hicho.

Kauli hiyo inatokana na chama hicho kugomea uchaguzi wa marudio uliotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na kufanyika tarehe 20 Machi mwaka huu baada ya kufuta matokeo halali ya uchaguzi wa mwaka jana unaotajwa kumpa ushindi Maalim Seif.

error: Content is protected !!