April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif ajitosa Serikali za Mitaa

Maalim Seif Shariff Hamad

Spread the love

MABADILIKO kamili katika siasa, uchumi na kijamii hayawezi kufikia iwapo wananchi watasita kwenda kujiandikisha ili kupiga kura. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Maalim Seif Sharif Hamad, Mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo leo tarehe 9 Oktoba 2019, siku moja baada ya zoezi la uandikishaji wapiga kura linaloendeshwa na Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuanza.

Mwanasiasa huyo nguli na Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Wananchi (CUF), amewataka Watanzania kujiandikisha ili wapate fursa ya kuchagua viongozi wapya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa Nonemba mwaka huu, watakaoongoza katika kwa mitano (2019- 2024).

“Tujiandikishe tafadhari. Usikose kujiandikisha na kuwa sehemu na kushiriki kikamilifu kuleta maendeleo tuyatakayo Tanzania,” amesema Maalim Seif na kuongeza.

“Tumepata fursa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi wapya katika kipindi cha miaka mitano. Tujiandikishe.”

Zoezi hilo linafanyika kwa muda wa siku saba, kuanzia tarehe 8 hadi 14 Oktoba 2019.

Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu, ambapo Watanzania watachagua viongozi wa serikali wa vijiji, vitongoji na mitaa.

error: Content is protected !!