January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif ajitangazia ushindi

Spread the love

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ameitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutangaza matokeo ya kura ya urais visiwani humo. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Taarifa iliyoandikwa na Shirika la Utangazaji Ujerumani-DW imemnukuu Maalim Seif akisema baada ya chama chake kukusanya fomu zote za matokeo kutoka vituoni, yeye amepata kura nyingi.

“Baada ya kukusanya matokeo yote, nimepata kura 200,007 dhidi ya kura 178,363 za mgombea wa CCM anayetetea nafasi yake, Dk. Ali Mohammed Shein.”

Maalim Seif ameitika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo halisi kama yalivyo kwenye fomu zinazotoka vituoni.

error: Content is protected !!