MAALIM Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) amesema kuwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) sio chama cha kukimbilia. Anaripoti Regina Kelvin …(endelea).
Amesema, haoni sababu mtu mwenye msimamo imara kukimbilia kwenye chama hicho na kwamba, mfumo wa uendeshaji wake haukidhi wara kuridhisha.
“Siridhishwi hata kidogo na utendaji wa CCM” amesema Maalim Seif alipokuwa Kilimahewa visiwani Zanzibar wakati akizindua Jumuiya ya Wazee wa chama hicho (JUZECUF) jana.
Amesema kuwa, hana ndoto ya kujiunga na CCM ambayo utendaji wala mwelekeo wake kwa taifa hauelewiki.
Maalim Seif ameeleza kuwa, kinachotokea katika serikali inayoindwa na CCM hasa kukamatakamata hovyo hakijawahi kutokea hata wakati wa Ukoloni.
“CCM inatakiwa kuelewa haiwezi kutawala nje ya mfumo ambao Watanzania wanavyotaka nchi yao itawaliwe,” amesema na kuongeza;
“Mara kwa mara unasikia diwani ama mbunge kaingia CCM, tena kwa kutoa tamko maalumu. Haya mliyaona wapi?” amehoji Malim Seif.
“Imefika hatua sasa Mwenyekiti wa Kijiji kwa kuwa tu anatoka CCM basi anaweza kuamrisha Jeshi la Polisi likukamate na unakamatwa kweli na kuwekwa ndani,”amesema Maalim Seif.
Katika mazungumzo na wazee hao Maalim Seif amegawa kadi kwa wanchama wapya huku akiahidi kuendelea kuimarisha chama hicho.
Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...
By Mwandishi WetuJune 1, 2023Spread the love IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...
By Saed KubeneaJune 1, 2023Spread the love SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...
By Mwandishi WetuMay 31, 2023Spread the love RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...
By Mwandishi WetuMay 31, 2023
Leave a comment