May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif afikisha siku ya tisa hospitalini

Maalim Seif Sharrif Hamad, Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Spread the love

 

MAKAMO wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, bado anaendelea kupata matibabu katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja, Visiwani Unguja. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Maalim Seif, amelazwa hospitalini hapo tangu tarehe 26 Januari 2021, akielezwa kuugua maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19).

Katibu wa Maalim Seif, Issa Kheri Hussein, ameeleza MwanaHALISI Online, jana Jumatano tarehe 3 Februari 2021, kuwa bado kiongozi huyo yuko hospitali akipatiwa matibabu.

“Mimi ni katibu wake private (binafsi) wa ofisi. Siyo msemaji wa masuala yake binafsi. Kwa sasa, nature (asili) yake ni Makamo wa Kwanza wa Rais na hivyo, taarifa zake ziwe authorised kutolewa (zitolewe na mamlaka). Lakini bado yupo hospitali, anaendelea na matibabu,” ameeleza Hussein.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar, Dk. Juma Mohammed, alipoulizwa maendeleo ya afya ya kiongozi huyo, haraka alisema, “sina mamlaka ya kulizungumzia.”

Taarifa kuwa Maalim Seif amelazwa hospitali kufuatia kuambukizwa virusi vya Covid-19, zilitolewa tarehe 31 Januari 2021 na Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo,  Ado Shaibu.

Ado alisema, Maalim Seif, mkewe Bi. Awena, pamoja na wanafamilia wake kadhaa, wamethibitika kuugua virusi hivyo.

Aidha, aliyepata kuwa waziri wa Afya katika serikali iliyopita ya Zanzibar, iliyoongozwa na Dk. Alli Mohammed Shein, Hamad Rashid Mohammed, alinukuliwa alisema, amejulishwa kuwa Maalim Seif yuko hospitali baada ya kushambuliwa na virusi vya Corona.

Waziri huyo wa zamani wa afya ambaye ni kiongozi wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), aliwataka wananchi kumuombea dua mwanasiasa huyo mkongwe Visiwani ili aweze kurejea katika majukumu yake.

Hata hivyo, pamoja na Maalim Seif, kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUKI), siyo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wala Serikali ya Jamhuri ya Muungano, iliyotoa taarifa kuhusiana na ugonjwa wake

error: Content is protected !!