Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maadhimisho Uhuru yaahirishwa, JPM atoa maagizo
Habari za Siasa

Maadhimisho Uhuru yaahirishwa, JPM atoa maagizo

Jengo la Hospitali ya Uhuru inayojengwa na Serikali katika wilaya Chamwino, Dodoma
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Magufuli ameahirisha maadhimisho ya 59 ya sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara zilizokuwa zifanyika tarehe 9 Desemba 2020. Anaripoti Brightness Boaz, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Magufuli ameelekeza fedha Sh.835.4 milioni zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hizo zitumike kununulia vifaa mbalimbali kwenye Hospitali ya Uhuru jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu leo Alhamisi tarehe 3 Desemba 2020 imesema, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa taarifa hiyo kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) zilizofanyika jijini Dar es Salaam.

Majaliwa amesema, Rais Magufuli ameagiza siku hiyo itumike kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kijamii nchini.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua jengo la Hospitali ya Uhuru inayojengwa na Serikali katika wilaya Chamwino, Dodoma

Tarehe 20 Novemba 2018, Rais Magufuli aliagiza kiasi cha Sh.995.18 milioni zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya maadhimisho ya 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, zitumike kujenga Hospitali ya Uhuru, ambayo kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 92.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya 59 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa mwaka 2020 inasema; ‘Miaka 59 ya Uhuru na Miaka 58 ya Jamhuri: Tanzania yenye Uchumi Imara Itajengwa na Watanzania Wenyewe, Tufanye Kazi kwa Bidii, Uwajibikaji na Uadilifu.’

Waziri Mkuu amesema, hadi kufikia sasa ujenzi wa hospitali hiyo ya Uhuru umegharimu Sh.4.2 bilioni.

Januari 2019 wakati akipokea gawio la hisa za kampuni ya Simu ya Airtel, Rais Magufuli aliagiza kiasi cha Sh.2.41 bilioni zilizotolewa na kampuni hiyo zitumike katika ujenzi wa hospitali hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!