Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Maabara Kibong’oto kufikia ngazi ya nne
Afya

Maabara Kibong’oto kufikia ngazi ya nne

Spread the love

 

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amemuahidi Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango kuwa maabara ya afya ya jamii ya Kibong’oto baada ya muda itafika ngazi ya 4 itakayoweza kutengeneza chanjo ya magonjwa mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Waziri Ummy amesema hayo leo tarehe 16 Julai, 2022 katika uzinduzi wa Maabara hiyo iliyopo katika Hospitali jya Kibong’oto Wilayani Siha.

Maabara hiyo inayotegemewa kupima sampuli ya magonjwa mbalimbali ambukizi .

“Hapa nchini kwa sasa zipo maabara mbili za namna hii ambayo ni hiyo ya Kibong’oto na ile ya Dar es Salaam. Napenda kuwatoa hofu watanzania kwamba hivi sasa nchi ina uwezo wa vifaa na wataalam wa kupima sampuli za magonjwa magonjwa mbalimbali ambukizi,” amesema.

Waziri Ummy ameongeza kuwa Maabara hiyo haitajikita tu kwenye TB bali magonjwa mengine ya kuambukiza kama Chikungunya, Murbug, UVIKO-19 na mengineyo.

Waziri Ummy amesema hivi sasa wagonjwa wa TB wamepungua ambapo mwaka 2015 kati ya watu 100,000 kulikua na wagonjwa 306 na mwaka 2021 kati ya watu 100,000 kulikua na wagonjwa 222 sawa na upungufu wa 54%.

Kuhusu vifo vitokanavyo na TB Waziri Ummy amesema Mwaka 2015 kulikua na vifo 56,000 kati ya watu 100,000 ambapo mwaka 2021 kulikua na vifo 26,800 kati ya watu 100,000 sawa na upungufu wa 52%.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!