January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maabara Ilemela yatafuna bilioni moja

Ujenzi wa maabara mjini Ilemela

Spread the love

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela, mkoani Mwanza imetumia zaidi ya Sh. bilioni moja katika ujenzi wa vyumba 24 vya maabara kwenye shule 18 za Sekondari wilayani humo. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Henry Matata, amesema hayo wakati akivunja baraza la Madiwani, ambalo limefikia mwisho wake kwa mujibu wa sheria, huku akisema fedha zilizojenga mabara hizo ni makusanyo ya ndani na michango ya wananchi.

Matata ametumia nafasi hiyo kuwaomba radhi madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) wa kata za Kirumba, Nyamanoro na Ilemela, aliowasimamisha kwa muda wa miaka miwili na miezi mitatu kwa madai ya kutohudhuria vikao vitatu bila taarifa.

Amesema licha ya kuwasimamisha madiwani hao kwa muda huo kutohudhuria vikao hivyo lakini walirejeshwa katika dakika za mwisho mpaka wanavunja baraza hilo madiwani wote watatu walikuwepo.

Mmoja wa Madiwani waliosimamishwa, ambaye hakutaka jina lake kuandikwa kwenye gazeti, amesema sababu zilizosababisha wao kusimamishwa ilitokana na ufuatiliaji wao wa matumizi ya fedha za wananchi.

Hata hivyo amesema baada ya kuonesha msimamo wao katika baraza la madiwani, Meya huyo alitumia mwanya wa nafasi yake kuwasimamia ili kuendelea kutumia fedha za wananchi vibaya na madiwani wa CCM.

“Mimi na wenzangu tulisimamishwa kutokana na msimamo wetu pamoja na kumbana Matata kwa matumizi mabaya ya fedha za umma, kiongozi yeyote ambaye hataki kukosolewa huyo hafai, sasa Wananchi wanatakiwa kuwakimbia watu aina yake,” amesema.

Amesema ifike mahala wananchi kuwapima madiwani na wabunge wao walichokifanya katika kipindi chao cha uongozi, ili kuchagua viongozi ambao ni wa chapa kazi na wenye uchungu na maisha ya wapiga kura wake.

error: Content is protected !!