Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ma RC: Wanaume 22, wanawake wanne
Habari za Siasa

Ma RC: Wanaume 22, wanawake wanne

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa 26 ya Tanzania Bara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uteuzi huo, umetangazwa jana Jumamosi na Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Kati ya wakuu hao wa mikoa, wapo waliohamishwa, waliostaafu na wengine ikielezwa kwamba watapangiwa kazi zingine.

Uteuzi huo ni mwendelezo wa Rais Samia, kupanga safu za viongozi, tangu alipoingia madarakani tarehe 19 Machi 2021, kuchukua nafasi ya Hayati Rais John Pombe Magufuli.

Mwanamvua Mrindoko- Katavi

Hayati Magufuli, alifariki dunia, jioni ya tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, iliyopo Makumbusho mkoani Dar es Salaam na mwili wake, kuzikwa nyumbani kwao, Chato, Mkoa wa Geita.

Kati ya wakuu wa mikoa hao 26; wanaume ni 22 na wanawake wanne ambao ni; Zainab Telack aliyeuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Lindi, anakwenda kuchukua nafasi ya Omary Zambi ambaye amestaafu.

Rosemary Senyamule- Geita

Kabla ya uteuzi huo, Teleck alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Pili, ni; Rosemary Senyamule, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, kuchukua nafasi ya Mhandisi Robert Gabriel, ambaye yeye amehamishiwa mkoa wa Mara.

Rosemary amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Zainabu Taleck- Lindi

Tatu; Queen Sendiga aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa, kuchukua nafasi ya Ally Hapi, ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora.

Sendiga, alikuwa naibu katibu mkuu wa chama cha upinzani cha ADC-Bara ambapo, katika uchaguzi mkuu uliopita wa tarehe 28 Oktoba 2020, aligombea nafasi ya urais wa Tanzania.

Nne; Mwanamvua Mrindoko, aliyeteuli kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi, kuchukua nafasi ya Juma Homera, ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya. Mwanamvua, amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Uvinza, Mkoa wa Kigoma.

Wakuu wa mikoa wanawake, walistaafu ni; Anna Mghwira wa Kilimanjaro na Dk. Rehema Nchimbi wa Singida huku Christine Mndeme aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma, yeye amekwisha teuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara.

Wakuu hao wa mikoa na wateuliwa wengine, wataapishwa Jumanne tarehe 18 Mei 2021, Ikulu ya jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 9:00 alasiri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!