Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa M23 wakubali kuachia ngome yao, wakutana na Uhuru Kenyatta
Kimataifa

M23 wakubali kuachia ngome yao, wakutana na Uhuru Kenyatta

Spread the love

 

VIONGOZI wa kundi la waasi la M23 wamekutana na msuluhishi wa kanda rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta, mjini Mombasa, ambapo wamekubali kuondoa wapiganaji wao kutoka jimbo la Kivu Kaskazini huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mkutano huo umefanyika baada ya wanaharakati wa eneo la mashariki mwa DRC kulitaka jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki(EACRF) kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya waasi wowote wanaolipinga jeshi la Kongo kitu ambacho kinaweza kuongeza mivutano zaidi.

Mkutano huo wa Mombasa umekuja wiki kadhaa baada ya waasi wa M23 kuomba kuelezea matatizo yao kwa Kenyatta, ambaye ni mpatanishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pia mkutano wa kimataifa kwa eneo la Maziwa Makuu (ICGLR) kujaribu kuleta usuluhishi mashariki mwa DRC.

Bertrand Bisimwa ni mwenyekiti wa M23 ameliongoza kundi hilo kwenye mkutano. Kundi la M23 lilitengwa katika vikao vya mazungumzo na serikali ya Kongo mpaka watakapo jiondoa katika maeneo yote wanayoyashikilia.

Taarifa iliyotolewa Alhamisi imesema M23 wametangaza nia ya kutaka Amani.

“Wakionyesha nia njema na utayari wa kufanya kazi kuelekea suluhisho kwa hali ya eneo la Kivu Kaskazini, viongozi wa M23 wamekubali kuendelea na utaratibu wa kujiondoa kwa kuzingatia usitishaji wa mapigano.

Huko Kivu Kaskazini, waasi wa M23 wamkeondoka kutoka mji wa Kibumba na kambi ya Rumangabo. Lakini jeshi la Kongo linadai maeneo zaidi, wakiwashutumu waasi kutoa taarifa za uongo kwenye jumuiya ya kimataifa na watu wake.

Aidha, huko Kivu kaskazini asasi za kiraia zimetoa kauli ya mwisho kwa EACRF “ kuwashambulia waasi” Wanaharakati wanatishia kuanzisha maandamano dhidi ya uwepo wa wanajeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kama ilivyofanya kwa tume ya UN ya kulinda Amani Julai 22.

Mawasiliano ya mkutano wa Mombasa pia yamesema “viongozi wa M23 wamemsihi raisi Kenyatta kusaidia kuhakikisha kwamba kuna usalama ndani ya DRC na haki za raia zinazingatiwa na kutambuliwa, na pia majeshi yote ya ndani na nje yanayopigana mashariki mwa DRC yanaweka silaha chini kusimamisha mapigano ya aina yoyote au mashambulio dhidi ya M23 na kutafuta suluhisho la mzozo huo kwa njia ya Amani.

M23 pia imekubali kuendelea kuheshimu na kushirikiana na jeshi la nchi za Afrika Mashariki ambalo kwa sasa wameanza kudhibiti maeneo ambayo yameachiwa na M23. Mchakato huu uanedana na uamuzi mzuri wa mkutano wa wakuu wa EAC uliofanyika Bujumbura tarehe 8, Novemba 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!