MWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mzee Sylvester Masinde amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema, Mzee Masinde amefariki dunia alfajiri ya leo Jumatano, tarehe 15 Machi 2023.
“Tunasikitika kutangaza kifo cha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama, Mzee Masinde, kilichotokea alfajiri ya leo katika Hopsitali ya Rufaa Bugando, Mwanza, alikokuwa amelazwa. Tunatoa pole kwa familia, ndugu jamaa na wajumbe wa bodi kwa msiba huu mzito,” imesema taarifa ya Mrema.
Taarifa ya Mrema imesema kuwa, ratiba ya mazishi ya muasisi huyo wa Chadema, itatolewa baada ya chama hicho kufanya kikao na familia yake.
Leave a comment