June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lyimo ahoji utatuzi kero ya maji Dar

Wanawake wakichota maji

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Susan Lyimo (Chadema), ameitaka Serikali kueleza ni lini itatatua tatizo la upatikana wa maji ya uhakika katika Jiji la Dar es Salaam. Anaadika Dany Tibason … (endelea).

Amesema “serikali imekuwa ikipiga danadana juu ya upatikanaji wa maji huku yakiwepo mabomba mengi ambayo yamepasuka na kumwaga maji hovyo”.

Lyimo amefafanua kuwa katika Wilaya ya Kinondoni na zingine, tatizo la maji limesababisha akina mama wengi kutofanya shughuli za maendeleo kutokana na kutumia muda mwingi kupanga foleni kwa ajili ya kutafuta maji.

Kauli hiyo ameitoa bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza akiitaka serikali ieleze ni lini itaweza kutatua tatizo hilo jijini Dar.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Josephine Genzabuke (CCM), alitaka kujua ni lini serikali itapeleka fedha za miradi ya maji katika Wilaya ya Kasulu ili iweze kukamilika kwa wakati.

Akijibu swali la nyongeza la Lyimo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kasimu Majaliwa kwa niaba ya Waziri wa Maji, amesema ni kweli katika jiji la Dar es Salaam kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa maji.

Hata hivyo, amesea kutokana na hali hiyo, serikali inafanya jitihada za kuhakikisha inatatua tatizo hilo kwa kutumia mradi wa maji wa Ruvu juu na Ruvu chini huku ikiondoa miundombinu chakavu na kutandaza miundombinu mipya.

error: Content is protected !!